Siku moja moja Ankal kumbe hupigaga pamba kiaina... Hapa  akila swagga na mai beta-hafu wake kwenye Red Carpet wakati wa Shear Charity ball hoteli ya  Movenpick jijini Dar  weekend ilopita kusaidia kinamama walio na ugonjwa wa Fistula pamoja na kusaidia ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka katika Hospitali ya Amana

Ankal akiwa na Meya wa Manispaa ya Ilala Mstahiki Jerry Silaa (kulia) na Mh Diwani.
Chonde chonde wasukutuaji, mipasho nouma...!!
Picha na Shamim Zeze wa 8020 Fashions. 
Kwa mapicha ya kumwaga
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Ankal hiyo suti sio ya bongo, utakuwa umepewa na nanihii kama zawadi! Imekupendeza hiyo design itakuwa ya ulaya alafu nimekuona na wewe unazo kama 15 hivi kwa mshahara wako ukichanganya pamoja na wa blog huwezi ukawa na suti za bei mbaya namna hii! kuna mkono wa mtu hapo! Tuambie mshonaji ni nani?? hahahaaa I like to mess with you ankal umetoka bomba suti imekukaa vizuri! ankal oyeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. uncleee KIATU chako tu, safi sanaaa!!!! unajichanganya kila sehemu

    ReplyDelete
  3. Ankal walaigh umechomoka ile mbaya, kumbe huwa unamvuto kiasi hichoooo, naomba niwe mgombea mwenza na mai wifu wako ntakuwa radhi kuwa hata mke wa .......

    Umetoka bomba mbayaaaaaaaaaaaaa mwaaaaaaaaaaaaaaaah!

    ReplyDelete
  4. Ankal hapo juu Mkono huo wa kushoto umekamata nini tena? Ankal kwa konoz unatisha. Konoz kama zina sumaku vile. Hiyo suti nimeikubali Ankal, hebu kuwa muungwana na umsaidie huyo anayeziuza au kutengeza kwa kumtangazia hapa kuwa anapatikana wapi? Fanya uungwana tu humu duniani dill ni kusaidiana mtangazie biashara tafadhali Ankal.

    ReplyDelete
  5. Ankal, si unaona ulivyopendeza? Pendeza ankal achana na ile t-shirt yako ya mistari.

    ReplyDelete
  6. Ankal unamatatizo ya kukamata wanawake wa watu viuno. wanaita "pervert"!

    ReplyDelete
  7. Leo mie sina ugomvi na wewe, suti imekukaa siyo ile ya siku ile bungeni kuuuuuubwa........hii sasa ndio yenyewe!

    ReplyDelete
  8. ankal na mai wifu mmependezaje!!!!!

    ReplyDelete
  9. hivi nimesahau au suit (koti) siku hizi lina vifungo vingapi 2,3,4 hebu nikumbusheni wa dau

    ReplyDelete
  10. Ankal mbona unaonekana kama umevaa bulleti proof ndani ya hiyo suti, unamuogopa nani wakati hii ni nchi ya amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...