Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utawala Bora
Mh. Mathias Chikawe
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kuridhishwa kwake na kiwango cha mafanikio kilichofikiwa katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokabili utekelezaji wa haki za binadamu nchini.


Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe alipokuwa Akiwasilisha Taarifa ya Tanzania ya Mapitio Maalum ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu mbele ya Kikao cha Kazi cha Baraza la Haki za Binadamu, Geneva, Uswisi. 


Waziri Chikawe alikieleza kikao hicho kuwa Tanzania itaongeza juhudi zaidi ili kuhakikisha kuwa changamoto zinazokabili utekelezaji wa haki za binadamu zinageuzwa kuwa fursa muhimu katika kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaendelea kuheshimiwa nchini.


"tumejizatiti kuhakikisha kuwa sera, sheria na mipango yetu kuhusu haki za binadamu inazingatia haki na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu" alisema Waziri Chikawe.


Aidha, Waziri Chikawe alieleza kuwa mojawapo ya vipaumbele vya Taifa katika kuboresha hali ya haki za binadamu nchini ni ukamilishwaji wa Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Haki za Binadamu unaokusudia kuwashirikisha wadau mbalimbali katika ngazi ya Taifa kwa ajili ya kutekeleza masuala mbalimbali yakiwemo maboresho ya magereza, elimu na utoaji wa elimu ya haki za binadamu vijijini.


Katika kikao hicho, wawakilishi wa mataifa mbalimbali waliopata fursa ya kuzungumza waliipongeza Tanzania kwa kuwa na rekodi nzuri ya kulinda na kuheshimu haki za binadamu. Sanjari na hilo, Tanzania ilipongezwa kwa kutimiza malengo ya Elimu ya Msingi kwa Wote miaka mitano kabla ya muda uliowekwa kukamilika wa mwaka 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...