Na John Kitime
Mwaka 1995, nikiwa najaribu kusambaza kazi za wanamuziki wa Tanzania kupitia kajimradi kadogo, mwanamuziki Innocent Nganyagwa alinijia na kunihadithia kuhusu mwanamuziki mpya wa Rap ambaye alikuwa tofauti na wasanii wenzie, kimawazo na hata jinsi ya sanaa yake ilivyo, na ndipo nikakutana na kusikia kazi ya MR2.
Muziki wake ulinifurahisha kwa sababu mbili ya kwanza alikuwa akitumia Kiswahili kilichoeleweka tofauti na wasanii wengi wa Rap wa wakati huo ambao walighani Kiswahili utadhani wameshuka leo toka Marikani, pili alikuwa na ujumbe mzito, ambao hata leo miaka zaidi ya 15 toka ulipotolewa bado una maana kwa jamii ya Tanzania.
Sishangai kuwa yeye sasa ni Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi. Lazima nijisifu kuwa sikukosea kuanza kusambaza kazi yake ya kwanza album ya NI MIMI. Angalia video hii kwa makini utakuta mengi aliyosema atatimiza alitimiza.
Tembelea pia
http://www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com/
Imetulia hii...
ReplyDeleteCLASSIC!!!!!!!!!
ReplyDeleteDaaamn....this was in '96....yaani huyu jamaa was way ahead of the game...politically and socially conscious MC...kama Chuck D was Public Enemy....safi Mh. Mbunge!
ReplyDeleteSafi sana.......jamaa kaanza harakati cku nyingi sana!!Message iko clear sana na kiswahili sanifu
ReplyDeletemc wa ukweli,sio msanii tu!alichokuwa akikifanya sugu ni zaidi ya muziki,ni harakati!nashangaa hivi vitot kama f.a amabavyo kwa njaa zao tu leo wanadiriki kumtukana kwasababu ya njaa zao(huku wakidhalilisha fani) ili kuwafirahisha mabwana zao.......mbav!!!
ReplyDelete