Home
Unlabelled
JK akizungumzia suala la uraia pacha kwenye hotuba yake ya DICOTA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mheshimiwa Rais, hizo sababu unazozitoa kuhusu pingamizi la Watanzania dhidi ya 'Watanzania' wengine ni za kweli? Sikatai kuwa kuna mjadala ila ni kwa sababu unazozitoa? Zipi ni sababu za msingi zaidi? Sijaridhishwa na hotuba yako, nilitegemea kujifunza kweli kweli kuhusu suala hili ila nalazimika kuendelea kujiuliza na kutafiti zaidi kadri ninavyoweza.
ReplyDeleteKwa kweli sijafurahishwa kabisa na hotuba ya JK na applauses (vicheko vya kishabiki) vya wana DICOTA. Hivi hizo sababu alizotoa, ukiachilia mbali ile ya katiba, zina ukweli au uzito kiasi cha kuziongelea akiwa mtu wa wadhifa mkubwa na dhamana kwa Watanzania wote, popote walipo duniani? Kwamba nyumbani hatutakiwi kwa sababu tutafaidika kote kote???! Sidhani wenzetu waliopo nyumbani wanaichukuliaje hii kauli, ila kwa kweli sijawahi kuwasikia wakitoa sababu ya namna hii. Ninachojua hofu kubwa iliyopo (kwa waliopo nyumbani na waliopo ng'ambo) ni kuhusu kulazimika kufungua mipaka kwa nchi zingine, na jicho zaidi likiwa juu ya suala la ardhi. Na hii sio sababu ya kubeza, sote tunapaswa kuitafakari na kujiridhisha kwa dhati kama ina mantiki au tuitupilie mbali. Kuna sababu zingine za msingi zaidi pia na sio kuwa waliopo nyumbani hawafurahishwi na sisi kurejea kama raia. Naona kama aliyoyasema JK yanaweza kusababisha chuki kati ya yetu (walipo nyumbani na waliopo nje), chuki ambayo siamini kuwa ilikuwepo kivile. Ni vema tuendeleze mjadala kwa hoja zitakazotupa majibu.
ReplyDeleteNajua kuna wengi watakaonichamba kwa niliyoyasema, nimejiandaa kwa hilo kwani ndivyo Watanzania tulivyo. Nitafurahi kujifunza zaidi kutoka kwa wenzangu wenye subira na nia ya kuelimishana.
Ankal, mara nyingi huwa unazitupa comments zangu ila naomba uithamini hii kwani ni vema wimbi la kuelimishana na kukumbushana lidumu kwa faida ya watu wote. Asante.
Suala la duo citizenship ni gumu kuliko mnavyofikiria ninyi mnaolitaka. Watanzania sio kwamba hawataki hilo jambo, la hasha, wanataka kwanza muwaambie faida za kuwa na huo uraia pacha. Ndio maana raisi anasema sababu mnazozitoa zina maslahi kwenu tu ambao mmeshakwenda nje. Huo ni ubinafsi. Waelimisheni watanzania faida za kitu kama hicho kwenu na kwao pia. And the benefits should be tangible. Mtanzania wa leo hataki kudanganywa na vitu vya kufikirika. Kwa hiyo ningewashauri ninyi mnaolilia suala hilo mfanye utafiti wa kutosha kuhusu faida na hasara za kuwa na uraia pacha kwenu ninyi mlio nje ya nchi, kwa watanzania waliopo nyumbani na kwa taifa zima kwa ujumla. Kama utafiti wenu utatuonesha faida ni kubwa kuliko hasara basi hakuna atakayepinga. Na utafiti huo ndio mtakaoutumia kuishawishi serikali na wananchi wake kuhusu kuridhia jambo hilo. Sio suala la kuongelewa kwenye risala tu mkafikiri maamuzi yatachukuliwa.
ReplyDeleteMdau, Australia
Mdau Australia uko na point lakini pia faida nafikiri zinaonekana hivi sasa kabla ya kufanikisha hilo swala nyumba zinajengwa,watu wanasaidia ndugu zao na michango mingi kusaidia serikali na pia michango mingine kwa wanafikwa na maafa!sasa vikwazo kwa sisi ambao tunaishi nje haturuhusiwi hata kufungua Acount pale nyumbani na tuko na majumba na miradi yetu na viza tunapewa haitoshelezi kwa kukaguwa miradi yako sasa unajikuta unawafaidisha ndugu na pia kujenga uhasama kwa wanandugu wale ambao wanataka kula bila kuangalia maendeleo ambayo pia yangemfaidisha mtanzania mwengine!wakati akija mwekezaji anapewa mkopo palepale kwetu kwa sbb ameingia kwa sura ya uwekezaji sasa watanzania tuliotoka nyumbani hali zetu nizakuchanga unajituma huku utengeneze nyumbani lakini pia unabanwa wakati wenzetu nchi nyingine wanaambiwa ukiipata hata bolt itupe nyumbani itasaidia!Na pia sisi tukipewa kipa umbele uchumi unakuwa kwa sbb yakutuma pesa nyumbani benk zinapata kazi na hata bured change yaani kwakweli iko mianya mingi sana yakufaidika tanzania ikifanikisha hili swala kulikoni kwa huyo anapewa hiyo duel!na ndio maana wenzetu wa nchi nyingine hawakuona kama hili swala ngumu lakini sisi watanzania nikwamba tuko na choyo na wivu tu ndio kitu kinatusumbua!Na kaka yangu ama dada uliesema unajuwa utachambwa kwakweli umeongea poinnt nzuri usiwe na wasi.
ReplyDeleteMimi kwa mtizamo wangu iundwe komitee ambayo itatowa watu wa dacota na diaspora iende nyumbani ikaelimishe watanzania wenzetu ilikuwatowa hofu ndio kitu kizuri!
Kwa ufupi ili ukubalike kuwa mwekezaji au muhamiaji halali inabidi uwe umefuata masharti ambayo kwa waTZ ambao wameshachukua uraia wa nchi nyengine wengi wao hawawezi kutimiza. Labda njia mbadala ni kuwa kama babu au bibi ni mTZ mtu anaweza kuruhusiwa kufanya kazi na vitu vyengine kama hivyo. Lakini urai wa TZ wa nini wakati wewe una uraia wa UK au USA? Kwanini usiwekeze huko UK au USA? Vidola ishirini elfu havitoshi kutupotezea muda na kukupa uraia wetu, itabidi uje ujiripue tena bongo!!
ReplyDeleteNi very simple kuelewa faida na wala sio suala la ubinafsi kama inavyotafsiriwa.
ReplyDeleteIwapo Watanzania walioko nje wataweza kupata baadhi tu za faida chache kama zilivyodokezwa mfano elimu bure, gharama nafuu za nyumba, matibabu bure, mikopo mikubwa, investment opportunities ng'ambo kama raia nk, hii ina maana kuwa watanzania hawa wataweza ku-save pesa nyingi sana kwa maendeleo ya nyumbani pia.
Kwasasa ni kwamba Watanzania wengi walioko nje kwa sasa wanashindwa kufikia malengo au kutuma pesa nyingi nyumbani kwani inabidi pesa hizo ndio watumie kwa gharama kubwa katika elimu, nyumba,matibabu nk, vitu ambavyo wangevipata bure au kwa gharama nafuu zaidi.
Tuangalie baadhi nchi za wenzetu za Afrika wako mbali. Watu wanaishi ulaya marekani kwa lengo moja tu, "Kuchuma" na baadae warudi nyumbani. Hakuna mwafrika anayependa kuzeekea au kufia ulaya nk. Hakufai. Ndio maana watu wanaishauri Serikali itafutie ufumbuzi uraia pacha.
Nimesikitika sanasana kusikia eti wanasema hawataki kuona watu wanafaidika kotekote! Hivi kweli watanzania kweli bado tuna hizi fikira ktk karne ya leo??? Ni aibu kubwa kusikia! Tuache roho ya kwanini, imepitwa na wakati. Mmoja wetu akifanikiwa tumuunge mkono kwani ndio mwanzo wa kulinyanyua taifa.
Na pia kwa nini inaonekana maamuzi ya suala hili bado kufikiwa na imekuwa kama porojo tu since then?
Jamani tuna Bunge, ni jambo la kukaa chini taratibu zifutwe kipengele cha katiba kuhuru uraia kifanyiwe marekebisho. Tuache mambo ya kuongea miaka ndenda rudi, dunia inakimbia kwa kasi, tutaachwa zaidi kwani tayari tumeachwa.
Anonymous wa pili umeongelea suala la ardhi kama changamoto kwenye uraia pacha. Naungana na wewe. Lakini changamoto sio ardhi tu. Kuna mambo mengi kama vile tofauti za kiutamaduni, kiuchumi n.k.
ReplyDeleteAnony wa nne umeongelea benefits kama vile kujenga nyumba n.k. Wote mna mawazo mazuri. Lakini haya yote mnatakiwa myaweke kwenye reserach report. Mimi ushauri wangu bado unabaki kwamba kufanyika utafiti wa kina ndio njia pekee itakayotuwezesha kukubali ama kutokubali uraia pacha. Wazo la anony wa nne kwamba iundwe committee ikawaelimishe watanzania linaweza lisiwe na tija sana kwani litakuwa la kisiasa zaidi. Wanaweza wakaelimishwa na wakakubali kulingana na umahiri wa mjenga hoja. lakini kumbukeni hili ni jambo lenye maslahi kwa taifa kuanzia kizazi cha leo, kesho na keshokutwa. Leo hii tunaweza kujenga hoja kuwa lina faida tukalisemea kwenye majukwaa mbalimbali tukataja na mifano miwili mitatu ya faida na mtanzania wa leo akatuelewa. Kesho watoto na wajukuu wetu watakapokuwa wamesoma na kuja kugundua jambo hili limechangia kwenye matatizo yao, watatuona sisi baba na babu zao kuwa tulikuwa hatuna akili.
Mnajua kama mtu una data/facts unaweza kuzitumia kushawishi watu wengi zaidi kuliko mdomo peke yake. Naamini kwenye research kuna mambo mengi yataibuliwa (mazuri na mabaya) kuliko wengi tunavyofikiri.
Mngeweza mkafanya research hiyo kwa kuangalia mambo yafuatayo:
1. Ni nchi ngapi duniani zinatumia mfumo huo?
2. Zipi ni faida wanazo zipata
3. Zipi ni changamoto wanazokumbana nazo na wanatumia mbinu gani kukabiliana na changamoto hizo?
4. Je watanzania tuna uwezo wa kukabiliana na changamoto kama hizo endapo zitatokea kwetu?
n.k
Kuwatuhumu tu watanzania kuwa wana choyo bado haitoshi kuleta uraia pacha. Sanasana kauli kama hizi zina ukweli lakini zinaweza kuwa chanzo cha migongano katika kujadili suala hili.
RAIS NA MARAISI WAJAWO,,,,KUNA HUMUIMU WA KUBADILISHA MAMBO MENGI YA KUHUSIANA NA KATIBA YA NCHI,,,,,DUNIA INABADILIKA NA SISI TUBADILIKE KAMA WATANZANIA,,,SWALA LA URAIA NI SWALA LA GLOBAL CHANGE ,,,NA SISI TUCGANGE AS COUNTRY KWA UDUMA YA WATANZANIA,,,SWALA LA TOURISM TANZANIA TUNALIUWA WENYEWE KWA GREED AND SELFNESS ,,,,WATU WENGI WATANZANIA WANAJALI SANA MATUMBO YAO ,,,,SELIKALI YA TANZANIA MUWE NA UWEZO WA KUBADILI KATIBA YA NCHI KUFATWANA NA WAKATI NA RISK YA VITU VINAVYO BALISHWA,,,,,CHUO KIKUU NA WANA MIUNDO MBINU WANATAKIWA WAWE UPDATE NA WORLD KATIKA KAZI ZAO SIYO KUKAAA TU MAOFISINI MNAKURA TAXPAYER MONEY ,,,DUNIA INAPOKENDA SIYO YA SERIKALI ZA KIKOLONI WATU WANASOMA NA WAKO TAYARI KUIBADILISHA TANZANIA ,,FROM TAXATION,ROAD,PROPERTY TAX,LAWS AND SECURITY AND LESS EXPENDITURE,,,NA KAMA KUNA WAZEE WANAOJIFANYA WAO WAMECHANGIA KULETA HURUHU NA WANAHAKI YA KUFANYA KILA KITU ,,NO NO NO THAT'S NOT RIGHT AS TANZANIAN ,,,,TANZANIA NI NCHI YETU NA SISI NDIIYO TUNAETUNGA SHERIA NAAMINI AKUNA KITU CHA KUSEMA AKIWEZEKANI EVERYTHING POSSIBLE ,,TUSILETE SIASA NYINGI KWA KUWAUMIZA WANGI WALIO NA HALI YA CHINI,,,,,,TUNAITAJI DEMOCRASY YA KUTOSHA HILI TANZANIA HIENDEREEE (MOVE FOWARD)SWALA LA KATIBA NA KANUNI ZA NCHI ZIANGALIWE UPYA NA ZILEKEBISHE ACCORDINGLY AND TIME WE HERE NOW,,,,,,AB
ReplyDeletemimi ninaona mwenye pingamizi kuliko wote ni bwana kikwete. hizo reasons anazotoa zinanishangaza. kwani hizo nchi zote za africa zenye kuruhusu uraia pacha unafikiri hazikuwa na upingamizi fulani i am sure walikua nazo. kikweti has always been against hili jambo. kama kweli angelikua analiunga mkono kusingekua na problem. watanzania ngojeeni mpaka may be the next government
ReplyDelete