hivi sasa kuna gari moja la abiria lisilo na route maalumu lipo huku External makuburi na abiria wake wote, baada ya abiria hao kugoma kushuka wakidai wanataka kupelekwa kwao.
Sakati hili linaonyesha abiria hao wanaelekea mbezi na dreva wa daladala hilo alipakia mpaka kimara lakini abiria kugoma kushuka wakidai wapelekwe mbezi, ndipo dreva na konda wakaamua kuwarudisha ubungo ili wawarudishie nauli lakini abiria hawa wamegoma kushushwa. Ndipo dereva akaamua kulileta gari huku kwetu linapolala with FULL OF ABIRIA. Chakuchekesha zaidi abiria walipotaka mpiga dreva wanakijiji wa huku wametishia kuwa piga abiria kwani dreva ni mtu wa hapo kitaani.
Hivi sasa polisi wa kituo cha BUGURUNI wamefika na crusel yao mara baada ya askari ya external police post kushindwa kutatua tatizo. Na naona wamekubaliana gari liende URAFIKI.police.
Mdau Gango

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kweli Bongo tambalale..
    Kinachowasumbua ni ukosefu wa Elimu
    Hivyo ustaarabu hakuna kabisa.
    Hicho ndicho pekee cha kujivunia kwa miaka 50 ya uhuru.

    ReplyDelete
  2. Wewe mdau wa hapo juu nani aliyekosa elimu hapo au nani si mstaarabu?

    Fafanua tuelewe ni dereva au abiria?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...