Waziri wa Nishati na Madini akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Nishati na Madini.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano la kimataifa la Nishati na Madini wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani).
 waziri wa Nishati na Madini akiwa kwenye moja ya mabanda ya washiriki wa kongamano la nishati na madini
 waziri wa Nishati wa Madini akiwasiliza kwa makini moja ya waoneshaji wa maonesho ya nishati na madini wajulikanao kama Protea Chemicals kutoka South Afrika.
 Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na washiriki kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL ambao walikuwa ni moja ya washiriki wa kongamano na maonyesho ya kimataifa ya nishati na  madini.
waziri wa Nishati na Madini akisalimiana na washiriki kutoka kampuni ya Geita Gold Mining.
 ======  ========  =======
Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja ameshiriki  kongamano la kimataifa la nishati na madini lililofanyika tarehe 19 na 20 ) Octoba, 2011 katika hoteli ya Ngurdoto Arusha.
 
kongamano hilo la siku mbili limeenda sambamba na maonesho ya nishati na madini na ni la kwanza kufanyika Tanzania ambapo zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali duniani wameshiriki.
 
katika hotuba yake Waziri wa Nishati na Madini alieleza changamoto zinazoikabili sekta za nishati na madini kama miradi mingi ya nishati na madini kuendeshwa kwa kutegemea fedha za wafadhili, kuyumba kwa uchumi kutokana na kubadilikabadilika kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na ukame.
 
hata hivyo alieleza kuwa Wizara inajivunia mafanikio mbalimbali ikiwemo utungwaji wa sera ya madini ya mwaka 2009 na sheria ya madini ya mwaka 2010 ambazo kwa pamoja zimewezesha Serikali kulipwa mrabaha wa asilimia nne toka asilimia Tatu kwa miaka iliyopita.
 
vile vile  sera na sheria  inaelekeza makampuni ya  uchimbaji madini kutakiwa kujisajili kwenye soko  la hisa ili wananchi waweze kununua na hivyo kuwa moja ya wamiliki kupitia hisa hizo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Naona sasa serikali inatukanganya, inakuwaje mkutano wa kwanza na wa aina yake ikijuisha maonyesho mbalimbali ya nishati na madini, sisi wananchi tusipewe taarifa uwapo wa huo mkutano ili tushiriki kuona hay yaliyoonyeshwa.... au ni maonyesho kwa ajili ya mh. WAziri tu?
    Pili kufanyia huko nguldoto inamaanisha nini , maana ni mbali kufikika wa wananchi kuhudhuria hayomaonyesho..... hapo napata shaka kuwa sisi wananchi tunatengwa... na huo ni uhusiano wa serikali na wadau wawekezaji tu... Naomba serikali ijaribu kusikiliza vilio vya wanachi kuhusu madini na nishati isitufumbie mambo na sisi ni wadau wakubwa ... na ni wa lengwa pia.....rasilimali zetu zitufaidishe kama libya...

    ReplyDelete
  2. mzungu anamuogopa ngereja mpaka kalowa kwapa, usifanye mchezo kukutana na waziri, angekuwa kikwete huyo angelowa suruali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...