MAREHEMU KATHERINE LAWRENCE SAGUTI
(KETE)
Septemba 22, 1936 – Oktoba 4, 2009
Nakukumbuka mpenzi wangu. Wewe mama wa watoto wetu. Bibi jalili.
KETE
Tunakukumbuka jinsi ulivyokuwa mhimili mwema wa familia hii, mke mwema na mfano mwema wa imani ya Bwana wetu Yesu Kristo.
KETE, ulituhamasisha, ulijifunga nguvu kama mshipi kiunoni na mikono yako kuitia nguvu, hivyo kututia nguvu wote tuliokupenda. Ulituonesha upendo uliodhihirika kwa kazi zako na mwenendo wako mzuri,na karama katika upole wa hekima, na wengi walijifunza kwako.
Ulipendezwa na ufahamu, ukamtumaini Mungu hadi kufa kwako
KETE, tunaona ni kama jana tu yalipotokea haya. Lakini huu ni mwaka wa pili sasa, tangu ututoke machoni petu. Na hakuna siku inayopita bila kukukumbuka wewe na yote uliyotutendea. Hili linatufanya kila siku kufanya bidii ya kuyakumbuka, kuyaenzi na kuyatenda yale yote mazuri tuliyojifunza kwako.
Aidha, tunapata amani idumuyo tukijua ya kwamba, umetunzwa huko juu kwake Yeye ambaye anatufariji sisi huku chini, tukijua kuwa tutakutana tena, Yeye akiwa kati yetu; Yesu Kristo.
KETE mpenzi, unakukumbukwa sana na
Mumeo Mpenzi Lawrence,
Wanao na wajukuu pia.
Ufu 14:13- Nikasikia sauti toka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafao katika Bwana tangu sasa. Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Shangazi yetu tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi.Jina la Bwana lihimidiwe. AMIN
ReplyDelete