Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi akisikiliza maelezo kuhusu Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Afisa Vijana, Bw. Florens Karist wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa upande wa Wizara hiyo yanayoendelea Kijijini Butiama Mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akielezea jambo wakati alipotembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (katikati) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara nyumbani kwake Butiama Mkoani Mara. Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanazania Bara kwa upande wa Wizara hii zinazoendelea Katika viwanja vya Joseph Kazurira Nyerere kijijini Butiama. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu, Bi. Sihaba Nkinga na kulia kwake ni Diwani wa Kata ya Butiama Mhe. Peter Wanzagi.
Napenda sana kumuenzi baba wetu wa taifa ila nina wasiwasi tutafika sehemu mpaka familia yake watatuchoka sasa. Jamani inaonekana karibia kila siku mama Maria ana ugeni, anapata muda lini wa kupumzika??
ReplyDeleteNashauri tuwape muda na privacy hawa watu, nao ni familia kama sisi.
Mimi bado nina mashaka na dhana nzima ya kusherekea miaka 50 ya Tanzania. Hakuna nchi Tanzania iliyopata uhuru mwaka 1961, ilipata uhuru mwaka 1961 ni Tanganyika ambayo haipo. Tanzania au uite Bara au Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964. Huwezi kuongea Tanzania ukaiacha Zanzibar nje. Tukisema uhuru wa Tanganyika haipo ilishakufa kisiasa na kikatiba. Tukisema tanzania tuna maana Muungano wa Tanzania na Zanzibar sasa hiyo miaka 50 inatoka wapi? Wadau mnipe maana ya Tanzania na tofauti ya Tanganyika
ReplyDeleteNa hiki kitambaa ndio vazi la taifa au la wizara ya habari?
ReplyDeleteasante kwa habari zako ,zipo mbio kuliko za aina nanihii,sitaji naogopa mkong'oto,ila kichwa cha habari neno Tanzania linasomeka tofauti,rekebisha mitambo mkuu wa idara zote!
ReplyDeleteMohsein
Na sasa hivi Zanzibar walishang'atuka hivyo tuko kuleeee Tanganyika yaaani bado hatujapata uhuru,ndo maana hadi sasa hatuna uhuru wa kuongea tunanong'ona tu chinichini ili hali Kenya wanaongea liwalo na liwe ujumbe ufike. eeehe eeehe eeeeeeeeeeeh mdau umenichekesha sana kusema hakuna neno Tz
ReplyDelete