Askari wakimuongoza Rais wa Mozambiq, Armando Guebuza, kuelekea kuweka Shada la maua katika Kaburi la Mwasisi wan chi hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa nchini hiyo, Samora Machel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa Mozambiq, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19 mjini Maputo Msumbiji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na baadhi ya Marais wa nchi za Afrika wakati walipohudhulia katika sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa Mozambiq, Samora Machel, zilizofanyika leo mjini Maputo Msumbiji.
Kingunge Ngombale Mwilu, akijumuika na wananchi wa nchini Mozambiq, kuelekea kuweka mashada ya maua katika kaburi la Mwasisi wa nchini hiyo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa rais wan chi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Mozambiq, Mama Graca Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Mama Maria Nyerere akiweka Shada la Maua ndani chumba maalum mahala lilipo kaburi la mwasisi wan chi ya Mozambiq, wakati wa maadhimisho ya sherehe za kumbukumbu ya kifo cha mwasisi huyo zilizofanyika mjini Maputo Msumbiji leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...