Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto, akizungumza na Mama Maria Nyerere wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Familia ya Baba wa Taifa Hayati Malimu Julius Nyerere baada ya kumalizika misa maalum kwa ajili ya kumkumbuka Baba wa Taifa pamoja na uwashaji mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika kijiji cha Butiama jana. Katikati katibu wa Organaizeshen ya CCM Asha Abdalla Juma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Maria Nyerere katikati, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ujumbe uliomuwakilisha Rais Yower Museven wa Uganda kwenye Misa maalum ya kumkumbuka Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere iliyofanyika jana kijijini kwake Mwitongo Butiama.
Mbunge wa Musoma vijijini Mhe. Nimrold Mkono akijumuika na wasanii wa ngoma ya asili ya mkoa wa Mara kucheza ngoma hiyo, wakati wa sherehe ya kuwasha mwenge iliyofanyika jana katika kijiji cha Butiama mkoani Mara jana.
Vijana wa Halaiki kutoka Shule za mikoa mbalimbali ya Tanzania wakifanya Halaiki ya onesho la kijeshi wakati wa sherehe ya kuwasha mwenge iliyofanyika jana katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.Amour Nassor VPO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inapendeza sana kuona tunayafanya yale ambayo Hayati baba wa Taifa aliyafanya au kuyasisitiza yafanyike.

    "Daima tutakukumbuka na kukuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu JK Nyerere"

    ReplyDelete
  2. JAMANI HAYO MAANDAZI LOL! WE WILL ALWAYS REMEMBER YOU BABA WA TAIFA, NO ONE ELSE CAN DO WHAT U DID TO OUR COUNTRY AND NO ONE WILL EVER DO! MUNGU IBARIKI tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...