Wachezaji wa mpira wa magongo wa timu za Twigas (nyekundu) ya jijini Arusha na Magereza Tanzania wakimenyana katika mashindano ya Kombe la Nyerere yanayofanyika mjini Moshi.
 Hekaheka langoni mwa timu ya Magereza Tanzania.
 Mashabiki wakifuatilia pambano.
 Mlinda mlango wa timu ya Magereza Tanzania James Kayeko akijiandaa
kuondoa hatari langoni kwake.
Muandaaji wa mashindano hayo Inderjeet Rehal(wa pili toka shoto)akiwa na maofisa wa chama cha Hockey wakifuatilia pambano.


Na Dixon Busagaga wa 
Globu ya Jamii, Moshi.

TIMU ya mchezo wa mpira wa magongo (HOCKEY) ya Magereza Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Nyerere Cup yanayo fanyika katika uwanja wa Hindul Mandal ikiwa ni sehemu ya kumbukumbuya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere.



Mashindano hayo ambaye yameanza ijumaa iliyopita yanashirikisha jumla ya vilabu saba kutoka mikoa mbalimbali ambapo yanafikia tamati leo na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Moshi Musa Samizi.


Katika mchezo wa kwanza timu ya Magereza Tanzania iliichapa timu ya Moshi Kasa B kwa jumla ya mabao 2 kwa 0 kabla ya kuishushia kichapo timu ya Twiga ya Arusha kwa jumla ya mabao 4 kwa 2.


Katika mchezo mwingine timu ya Magereza iliadhibu bila huruma timu ya Kili vijana ya mkoani Kilimanjaro kwa jumla ya mabao 6 kwa 0 na kufanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali.


Akizungumzia ushindi huo afisa msaidizi wa michezo wa Magereza Matilda Mrawa alisema timu yake imejiandaa kuchukua ubingwa wa mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.Alisema timu ya Magereza imekuwa ikifanya mazoezi kwa muda mrefu huku ikiongeza wachezaji wapya ambao watasaidia kuipatia ubingwa mwaka huu.


"Hivi sasa huu mchezo una kua ,kwa sababu kila mwaka tunaposhiriki tunakutana na upinzania mkubwa kutokana na kwamba timu nyingi zimepata vijana wengi ambao kwa sasa wameanza kuujua vizuri mchezo huu."alisema Mrawa.


Alisema timu yake ina historia nzuri ya mchezo huo ambapo mwaka jana walifanikiwa kushika nafasi ya pili huku wakiibuka mabingwa katika mashindano ya muungano yaliyofanyika mwezi januari mwaka huu jijini Dar es salaam.


Kwa upande wake mwandaaji wa mashindano hayo Inderjeet Rehal alisema mashindano hayo yameendelea kukua siku hadi siku na kwamba mategemeo yake mwaka ujao mashindano hayo yashirikishe timu kutoka nje ya nchi.


Alisema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya kikombe na kila mchezaji atapatiwa zawadi ambayo itakuwa kumbukumbu huku mshindi wa pili akiondoka na kikombe pamoja na medali kwa kilamchezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Dixon, the event was held at the Sikh Club and not Hindu Mandal.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...