Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania aliefariki siku kadhaa zilizopita jijini Dar es Salaam kwa kuuwawa na majambazi wasiojulikana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,akiwa na viongozi mbali mbali kwenye ibada ya kumuombea Marehemu
Picha ya Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
Kamanda wa kanda maaluum ya kipolisi ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akiwapa pole wana jumuiya ya wachina waishio Tanzania jijini Dar es salaam wakati walipokwenda kuaga mwili wa Mama Han Bing alieuwawa na majambazi.
Wanajumuiya ya Kichina waishio nchini Tanzania wakiwa kwenye misa ya kumuombea Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole Mume wa Marehemu,Bw. Bing ambaye alikuwa ni mwenye huzuni mkubwa sana wa kuondokewa na mke wake aliyeuwawa na Majambazi siku kadhaa zilizopita.
Mama Salma Kikwete akimfariji Mtoto wa Marehemu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akitoa salamu za pole wa wafiwa na wanajumuiya ya kichina katika msiba huo.
Mume wa Marehemu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na wanafamilia wengine kwenye misa ya kumuombea Marehemu.
Mmoja wa Kina Mama wa Kichina akilia kwa huzuni baada ya kuondokewa na ndugu yao.
Mmoja wa wanafamilia akimbembeleza mtoto wa Marehemu.
Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nimesikitishwa sana na habari hii ya kuuawa kwa mke wa Kiongozi wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kichina. Kwa kweli naomba jeshi la polisi lifanye kazi ya kuwasaka hao majambazi waliohusika na mauaji hayo na kuwachukulia hatua kali za Kisheria. Maana bila kufanya hivyo wawekezaji kutoka nje watakuwa na mashaka na hali ya usalama wa Tanzania kupelekea kukwepa kuwekeza nchini.

    ReplyDelete
  2. tanzania tuna elekea wapi, i wish kama Mwalimu angekuwa hai ku witness watanzania tumegeuka nini!

    mdau paris

    r.i.p

    ReplyDelete
  3. Mimi kama mtanzania, nalaani kitendo hiki cha majambazi kuuwa raia wa kigeni. Nawapa pole ndugu zetu wa kichina katika msiba huu. Mwalimu Nyerere alitufundisha kuwa binadamu wote ni sawa. Hivyo naungana na ndugu zetu wa kichina kuomboleza msiba huu.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana wafiwa

    Kweli Tanzania kuzuri, sijawahi kuona wachina walionenepa kama hawa.

    ReplyDelete
  5. Nawapa pole sana hao wachina na tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu haswa ikizingatiwa ni wageni.Serikali isipojifunza kuwekeza kwenye usalama na afya ya watu Uwekezaji utavutia watu wachache sana.Dunia ya sasa watu wanaweka usalama na afya mbele hasa nchi zilizoendelea.kwa mauaji,ajali,na huduma mbovu za kijamii Tanzania kusonga mbele ni vigumu mno.

    ReplyDelete
  6. Ooooh No!Nimejikuta natoa machozi kwa kumuona huyu mtoto...age of my children...this is sooo mean!Mungu awape faraja ya ajabu huyu baba na mtoto wake aliekatizwa utamu wa mama katika umri mdogo kama huu.Jamani tunaelekea wapi?

    ReplyDelete
  7. Pole sana wafiwa na Mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu Hun Bing.

    ReplyDelete
  8. we askari hivi walishakuvua utrafikli? na ulikuwa mnoko!!!

    ReplyDelete
  9. Sorry ina maana ya wachina tu ndo inauma? Mbona huu unyama upo sana Tz na wananchi wakiwaripoti wakakamatwa wanafungwa siku 2 ya tatu tunao mitaani wakiwatishia wananchi?. Hivyo wananchi wanaogopa hata kuwaripoti tena maana Tz kosa la kuiba kuku ndo linafuatiliwa kuliko kuua esp. pale ambapo mhalifu ni tajiri. Du sikujua tunawachina wengi kiasi hiki. POleni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...