Jumapili, Saa 1 Asubuhi, Octoba 23 Viwanja vya mnazi mmoja, Dar es Salaam


Saratani ya matiti inagusa maisha ya kila mmoja wetu kupitia kwa wana familia wetu, marafiki, jirani zetu au sisi wenyewe. Sote tu majeruhi wa maradhi haya kwa namna moja au nyingine. Tuungane kusaidia mapambano haya. 

 Jiunge na matembezi ya Kilomita tano (5 km) ya Pink Walkathon ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wagonjwa na kwa malengo ya kuhamasisha uelewa mpana zaidi wa maradhi haya.  Baada ya matembezi hayo shiriki katika matukio ya ziada ya burudani yanayohusisha dansi, vinywaji na mengine mengi yanayohusisha ngoma na michezo ya watoto. 

Ada ya usajili ni shilingi 10,000 kwa watu wazima na shilingi 5,000 kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 8 – 15. Watoto wenye umri wa chini ya hapo wataingia bure. Fomu za usajili zinapatikana; Mlimani City (Kuna meza ya Volunteers karibu na ukumbi wa sinema wa Century) na jengo la LAPF Millenium Towers ground floor.

Fedha zitatumiwa na Mfuko wa Saratani ya Matiti (The Tanzania Breast Cancer Foundation)Kwa taarifa zaidi piga simu +255 22 276 2015/17 au tembelea wavuti katika www.tzbreastcancer.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...