Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba akimkabidhi bendera ya taifa Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika fainali za mashindano ya urembo ya Dunia yatakayofanyika jijini London Novemba 6. Mrembo huyo anatarajiwa kuondoka Oktoba 19. Kushoto ni Mkuu wa udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza na Mlezi wa kamati ya miss Tanzania, Emmanuel Ole Naiko. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.Picha na Francis Dande.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba akimkabidhi Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel kitita cha dola za kimarekani 1000 kwa ajili ya maandalizi ya safari yake ya kwenda nchini Uingereza kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya Dunia ya Urembo yanayotarajiwa kufanyika Desemba 3,2011.
Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel akizungumza katika hafla hiyo ya kumuaga.
Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel katika pozi
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Nakuala Senzia akimkabidhi Vodacom miss Tanzania Salha Israel dola za kimarekani 2000 kwa ajili ya safari hiyo.
Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel akizungumza katika hafla hiyo ya kumuaga.
Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel katika pozi
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Nakuala Senzia akimkabidhi Vodacom miss Tanzania Salha Israel dola za kimarekani 2000 kwa ajili ya safari hiyo.
Watanzania mimi napenda kuwaasa kwamba, mtu au nchi inapotumia pesa ya nchi nyingie ndani ya mipaka yake namna hiyo, ndo pale mnapo sababisha thamani ya pesa yetu kushuka, huyo binti alipaswa kupatiwa(kupewa) pesa ya Tanzania na siyo dollar kama inavyoonekana hapo, huko ni kutukuza utawala wa nchi nyingine ndani ya mipaka ya Tanzania, sijui nisemeje, kwasababu hilo halihitaji mtu kwenda chuo kikuu kusomea uchumi ni swaala la kawaida tu.
ReplyDeletekafanabna na nargis mohamed miss namba 2 sijui wa mwaka gani tena
ReplyDeletehivyo vitu ananunulia hapa, labda anaagiza ndo maana wamempa dollar, tusiwe tunakosoa hata vitu visivyokuwa na maana. Labda ingekuwa zawadi.
ReplyDeletesasa ndugu yangu mfano wangempa hizo shillingi angekwenda kuzibadilishia Heathrow au??
ReplyDeleteyaani umesema kweli kabisa, dola inapaa kutokana na sisi watanzania kutothamni pesa yetu, kila kitu dola, sasa hivi imekuwa kawaida hata kodi za nyumba kwa dola, shlingi inazidi kuporomoka! dah! hata sjui tuseme vipi ndio watusikie ! lakini ndio matakwa ya nchi za magharibi
ReplyDeleteushamaba na tukuza nchi za watu,ok mpeni pound kwakuwa britain hawatumii us dollar itabidi abadilishe hata huko,mdau wa kwanza upo sawa apewe tshs,
ReplyDelete