Hatimaye lile shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mara katika maswala ya utalii, litafanyika Ijumaa ya tarehe 07/10/2011, katika ukumbi wa Bwalo la Magereza mjini Musoma, ambapo takriban warembo 15 watapanda jukwaa moja kuchuana kumpata mwakilishi wa mkoa katika mashindano ya Miss Tourism Lake Zone yatakayofanyika baadae mwezi december. 


Kampuni ya Stoppers Entertainment inayoandaa mashindano hayo, imejipanga kuyapa hadhi mashindano hayo ambapo warembo mbali na kupita jukwaani, watashiriki katika shughuli za kijamii, kuimba na kucheza ngoma za makabila ya mkoa wa Mara. Hata hivyo waandaji wamewaomba wadhamini kuendelea kujitokeza kudhamini shindano hilo, kutokana na kugusa utalii, utamaduni na uchumi wa nchi yetu, yote kwa minaajili ya kuitangaza Tanzania.
Shindano la Miss Tourism Mara 2011, litasindikizwa na burudani kutoka kwa  Ditto na Linah wote kutoka jumba la vipaji THT. Pia burudani za ngoma za asili zitakuwepo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...