Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( aliyekaa kwenye kiti) akioneshwa sehemu inayokontroo masuala mbalimbali ya umeme baada ya kuvuliwa na kuingia kwenye gridi ya taifa kutoka mgodi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Kihansi, kutoka kwa Msimamizi mwandamizi wa uwezeshaji na usimamizi wa mfumo wa kompyuta , Christopher Mahundi (mwenye rula ) juu ya usimamizi wa matukio mbalimbali ndani ya mgodi huo Oktoba 14, mwaka huu.Picha na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sio MGODI bali MITAMBO ya kufua umeme.

    Kiswahili fasaha ingesomeka kama ifuatavyo:

    Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (aliyekaa kitini) akioneshwa sehemu inayodhibiti au ratibu masuala mbalimbali ya umeme baada ya kufuliwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa kutoka mtambo wa kufulia umeme wa Bwawa la Kihansi,.....

    ReplyDelete
  2. Huwa wanatumia neno MGODI kumaanisha hydropower plant

    ReplyDelete
  3. "Kufuliwa" - Mgodini; "Kuzalishwa" - Mtamboni. Kwa hiyo nyote wawili mwandishi wa kichwa cha habari na mrekebishaji hapo juu mnatuchanganya.

    ReplyDelete
  4. KUZALISHA WHAAAAT?????

    ReplyDelete
  5. Nilidhani Joel Bendera ni naibu waziri wa wizara ya michezo na utamaduni(samahani jina kamili la wizara hiyo silikumbuki). vipi imekuwaje leo ni mkuu wa mkoa?

    ReplyDelete
  6. Hufuatilii yanayoendelea nchini mwako anon unaeuliza kuhusu Joel Bendera?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...