Mpiga bezi wa Masondo Ngoma Jazz band akiwa kazini leo katika viwanja vya Leaders Club ambako Baba hawa wa Muziki nchini walifanya shoo kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wadhamini wa shoo hii ya bure walikuwa Tanzania Distilleries Ltd kupitia kilaji chao cha Konyagi
Waimbaji wa Msondo Ngoma wakiwa jukwaani
Jukwaa likishambuliwa vilivyo
Wana Msondo Ngoma kazini
Kiongozi wa Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo akitoa maelekezo kwa fundi mitambo
Ankal akiwa na wajina wake Mzee Gurumo ambaye alikuwepo kuongoza kikosi
Rapa Romanus Mng'ande 'Romario' (juu) akipozi na Mama Nzawisa na Omary Niachie Mimi
Wana Msondo Ngoma wakipozi na 'Mjomba' Muhidin Maalim Gurumo
Shaaban Dede akiongoza safu ya ushambuliaji
Kaka Cisco Mtiro akijikuna anapofikia
Kaka Cisco Mtiro akimtuza mpiga kinanda Ridhiwani 'Totoo'
Pangamawe baada ya kukunwa na Msondo Ngoma
Huwa nasema kila siku, hakuna mfano wa Msondo TZ.
ReplyDeletejamani hilo jukwaa linaogopesha, mtu aweza anguka maana laonekana kama c imara.
ReplyDeleteJamani huyo wajina wako ingefaa akaachana na mambo ya mziki sasa na akarudia mola..ni ushauri tu (qweman
ReplyDeletekaka nimefurahi sana kuwaona ndugu zangu wa msondo wakiendeleza libeneke,nimekumbuka sana bonanza la msondo tcc club jioni ya leo..lakini ndio hivyo tena niko ughaibuni kama mkibizi wa kiuchumi,namuona eddo sanga ,mdogo wangu hassan tx moshi(dogo anazidi kufanana na babake tx kila anavyokuwa),juma katundu,kakangu dede,kamanda gurumo,ridhiwani,zahoro bangwe,roma,bila kumsahau omari niachie mimi....wape salamu sana.
ReplyDeletemdau us