Kijana aliyetuhumiwa kuiba simu ya mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja,akipanda gari la polisi baada ya kumuokoa kutokana na kipigo alichokuwa akipata kutoka kwa wananchi wenye hasira kali mijini Songea jana,
Askari wa doria kutoka kituo kikuu cha polisi mjini songea wakimuokoa kijana aliyetuhumiwa kuiba simu ya mama mmoja ambaye hakufahamika,asiendelee kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali mjini songea jana,
Kijana aliyeshukiwa kuwa ni kibaka akiwa amelala chini kwa lengo la kuomba msaada baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kijana huyo kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ya mmoja wa wapita njia karibu na kituo cha daladala cha soko kuu mjini songea jana.
Kijana aliyeshukiwa kuwa ni kibaka akiwa amelala chini kwa lengo la kuomba msaada baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kijana huyo kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ya mmoja wa wapita njia karibu na kituo cha daladala cha soko kuu mjini songea jana.
Msamaria mwema  kulia ambaye hakutaka kutaja jina lake,akimuokoa kijana aliyekuwa akipata kipigo kutoka kwa watu wenye hasira kali,kufuatia kijana huyo kumuibia abiria simu ya mkononi katika kituo cha Daladala  cha soko kuu mjini songea jana,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ikifanikiwa kuiba simu moja kwa siku na kuiza 30 elfu tu basi kwa mwezi ana laki 9!!

    ReplyDelete
  2. Mob Justice is wrong! Yaani mtu kuiba simu ndio anapigwa namna hii? Waafrika tuacheni kuwa kama wanyama. Uhai wa binadamu una thamani kuliko bei ya simu.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa 12:45, nakuunga mkono sana. Watanzania hatujui madhara ya mob/vigilante justice. Mauaji ya Rwanda na Kenya hayakuanza kwa chuki ya siku moja. Ni watu kuona kwamba maisha ya mtu hayana thamani kama hivi simu/kuku/pochi n.k kuonwa sawa kabisa na kumpiga/kuumiza hata kuua mwenzetu.

    lakini naamini serikali, polisi, waziri wa afya na sheria, wanaharakati wote wanaona ni sawa maana sisikii kukemea kwa dhati. Hata wakisema. nadhani wanasema tu, lakini sidhani wanamaanisha.

    Tuendako ni kubaya! Yaani watanzania wana roho mbaya na za ukatili sana!

    ReplyDelete
  4. Cha ajabu ni kuwa anatuhumiwa, usishangae aliyetaka kuiba kakimbia, akina mama huwa wanapanic sana anawezakukuzushia wewe mwizi kwa kuwa upo karibu naye na haelewi aliyemwibia simu -na unaweza shangaa simu aliisahau nyumbani. yatubidi tubadilike looo.

    ReplyDelete
  5. Mob Justice is Wrong! Naskia mdau zamani ulikuwa kibaka?

    ReplyDelete
  6. we anon wa pili hujawhiibiwa eeh inauma sana , sawasawa dawa ni mkong'oto tuu unadhani huyu atafungwa?

    ReplyDelete
  7. How evident they are that the man was a thief. What if he didn't steal the phone, yet he has been injured/died? May we be logical than emotional decision making.

    ReplyDelete
  8. Mimi nauliza hao waliompiga huyo kibaka jee angekuwa ndugiyake amefanya kama hivyo kaiba angempa mkong`oto??? muogopeni Mungu jamani hiyo sio njia nzuri.

    ReplyDelete
  9. Nyie wote mliochangia naona mnakubaliana na waporaji. Nasikitika kuona hata hamjui kuwa ukimpeleka kibaka mahakamani hakuna hatua yeyote wanayochukuliwa wanaachiwa halafu wanakuja kukuua, vipi yeye akikuibia anakuponya au anakumaliza? Angalieni aliye mua yule mama wa kichina alianza taratibu tu. Mimi si watetei vile akiniibia probability yangu kuwa hai ni ndogo sana. Hivyo wapigwe hata kuchomwa moto akitoka hapo hatarudia na wale wenzie watakaokuwa wanamwangalia watapata fundisho.

    ReplyDelete
  10. we anonymous wa 2:27 kwani wanaoibiwa ni kina mama tu? Wacha uzushi eti akina mama hupanic na kuanza kupiga kelele kwani sisi vichaa?

    Of course mob justice siyo sheria hata kidogo lakini mbona wao wanakukaba wakikupata pembeni?

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana nyie wote mliosema mtu kupigwa kabla hajapelekwa kortini si haki. Kila mtu ana haki, kibaka vile vile, kusikilizwa halafu kupewa adhabu. Yaani ni Afrika tu unaona unyama kama huu. Ni lazima mmoja wetu awe mmpole, ingawa majambazi wanafanya vitu vya kinyama. Dai Lama alisema, ("eye for an eye leave a all world blind")Jicho kwa jicho utaacha ulimwengu mzima kipofu" nadhani nimetafsili sawa, niko tayari kusahihishwa.

    ReplyDelete
  12. Hivi wabongo tunaishi ulimwengu gani??? Hivi tnaona haya mambo ya namna hii ni sahihi kila siku? Kwanini watu wanajichukulia sheria mikononi tena kwa vitu vidogo vidogo? Yaani sisi tuna roho ya UKATILI kiasi hiki?? Kwanini tusimpeleke kwa vyombo vya sheria?
    Kama kweli tuko genuine na kuchukia wizi, kwanini basi tusianze kwanza na wanaoiba mabilioni ya nchi na kusababisha umasikini nchini?

    ReplyDelete
  13. hamjaibiwa nyie mkiibiwa mtajua uchungu wake , NINGEKUWA HAPO NINGEMPIGA KITOFAA, PAMBAFFFF !!!

    ReplyDelete
  14. jamani mnamuonea huruma huyu kibaka?ningekuwa hapo,ningempasua hayo mapumpu nitupie nguruwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...