Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mweyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi za Mbuga za Wanyama Tanzania TANAPA Bwana Modestus Lilungulu baada ya kukabidhi hundi ya thamani ya tsh.150m/- Milioni mia moja na hamsini ikiwa ni mchango wa Shirika hilo kwa ajili ya kujenga kituo cha wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam jana katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwaajili ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho zaidi ya Shilingi Milioni Mia saba zilipatikana ikiwa ni michango kutoka kwa watu binafsi,mashirika binafsi na ya umma.kulia nia makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Loooo! Kumbe inawezekana tukaachana na wafadhili tukafanya vitu vyetu wenyewe. kwa hili nakupongeza Kikwete, bravo!

    ReplyDelete
  2. Anko mbona hapo juu umeandika mkurugenzi wa TANAPA akikabidhi hundi ya 150M lkn hapo kwa mwisho unaconclude kuwa ni Tsh 7M zilipatikana au katika mahesabu hundi si pesa? Nauliza tu...

    ReplyDelete
  3. Inatia Moyo...

    Natumaini UDSM patabadilika na kuridisha heshima yake.

    peace, love & blessings

    ReplyDelete
  4. Anon,

    Naona umesoma sio sahihi, ameandika Milioni Mia saba. Na katika hizo niongezee, kulikuwa pia na hundi zingine na pesa taslimu (waandaaji watalifafanual hili baadae)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...