Kwanza kabisa tunapenda kuwasalimu wadau wote popote Duniani,tunatumaini ya kwamba bado mnaendelea na ujenzi wa taifa letu.
Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapa  taarifa kwamba mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo(www.tzwanavyuo.blogspot.com) sasa tumefanya mabadiliko makubwa ambapo tumewaunganisha wanavyuo watanzania wanaosoma Tanzania na walio Nje ya Tanzania.

 Tumefanya hivi kutokana na malalamiko na maombi ya Wanavyuo waliopo nje ya tanzania kutaka kuanza kutuma matukio yao ambayo yanajili huko waliko, Tumelipokea ombi hili na sasa mwanachuo yeyote ataweza kutuma habari zake ama habari zao hapa. 

Pia kwa watumishi wa vyuo Hapa nchini Tanzania mnakaribishwa sana kuleta matangazo yenu ikiwa ni nafasi za masomo ama kama kuna habari ya haraka mnataka iwafikie wanafunzi basi mtutumie moja kwa moja nasi tutaiweka muda huo huo. 

Mabadiliko mengine tuliyo yafanya kwa faida ya watu wote ni kwamba sasa tuna panel upande wa kulia ambapo tumeorodhesha tovuti za vyuo vyote vya Tanzania,pia tumeweka na mambo mengine mengi ya msingi ambayo yatapata kuwasaidia.Mtandao wa wanafunzi ambao unafanya kazi kama Facebook (Social network)upo hewani mnakaribishwa kujiunga
mnakaribishwa sana pia mtakutana na wanavyuo wengine.Tunatanguliza shukrani zetu za Dhati.

Tumumie matukio na habari zozote zihusuzo vyuo hapa:twanavyuo@live.com
Tembelea Mtandao wa Matukio na wanavyuo hapa:www.tzwanavyuo.blogspot.com
 
Kwa niaba ya wanavyuo wote,
Matukio na wanavyuo Crew.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...