Mwenyeketi wa Chama cha Wabunge wanawake toka Tanzania (TWGP) Mhe. Anna Abdalla (Mb) akimtambulisha Katibu wa Bunge Ndg. Thomas Kashililah (Mwenye Miwani) kwa ujumbe wa Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Zimbabwe wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Dar es Salaam. Ujumbe huo wa Zimbabwe upo nchini kwa ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu na wenzao wa Tanzania.
Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Zimbabwe (Mwenye Nguo Nyeupe) akieleza jambo wakati wa kikao cha Pamoja na Viongozi wa Chama cha Wabunge wanawake toka Tanzania (TWGP) walipotembelea Bunge jana. Ujumbe huo upo nchini kwa ziara ya mafunzo kutoka kwa wabunge wenzao wa Tanzania.
Picha ya Pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...