Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akipunga mkono wakati akiwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akiondoka nchini kwenda London Uingereza kushiriki fainali za Miss World zitakazo fanyika mwezi ujao.
Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Izrael (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  mrembo mwingine wa Miss Tanzania 2011, Blessing Ngowi (kushoto), Mama yake mzazi Sabrina Hamisi na Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo walipo msikindikiza kwenda London Uingereza kushiriki fainali za Miss World zitakazofanyika mwezi ujao. (Picha na www.mrokim.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ama kweli shangaa ya musa ya Firau'n huyawezi. Miskeen!

    ReplyDelete
  2. Mbona uswahilini naona wasichana wazuri zaidi ya huyu? Hawa wenye mashindano huwa wanatangaza muda gani applications maana mimi naona tuu picha za wanaoshiriki Miss Tanzania. But jinsi walivyochaguliwa haijulikani. I am sure tuna wasichana wazuri zaidi na wanaopenda kushiriki Miss Tanzania lakini sidhani kama wanapewa nafasi ya ushiriki.

    Hutu siwezi kutakia kila la heri kwa sababu kwa kumwangalia tuu sidhani kama atafika mbali. She will only remain Miss Tanzania, not Miss World

    ReplyDelete
  3. lol watu jamani. mbariki mwenzanko bwana ubarikiwe pia. hao wa uswahilini hawakusikia miss vitongoji au? ndio matatizo yetu wabongo hata kwenye kura ah mimi sipigi..akichaguliwa rais oh wamechakachua..hafai. ushuzi mtupu.
    Go Salha...Mungu akutangulie. Haters kama huyo hapo juu hawakosekani, stay focused. The 1 who cant do it, should not interrupt the 1 doing it.

    ReplyDelete
  4. Its always the question of ''technological know who'' that can make a young lady participate.
    We will never change...

    ReplyDelete
  5. mtoa maoni wa pili unaonekana kabisa una chuki binafsi

    kama huwezi kumtakia kila la heri hayo ni matatizo yako na roho ya choyo.

    na hao unaowaona ni wazuri kumshinda huyo hawajakatazwa kushiriki kwenye huo umiss

    sio kila mzuri anapenda kushiriki hayo mashindano wengine hawana mpango na mashindano kama hayo

    ReplyDelete
  6. Uzuri wa Miss Tanzania siyo wa sura kwani kuna vigezo vingi vyengine vinavyoangaliwa.

    Sasa wewe uzuri unalinganisha na nini? Kila mtu ana uzuri anaoangalia na siyo lazima vigezo vyako ndiyo viwe standard.

    Beauty is in the eyes of the beholder.

    ReplyDelete
  7. Loo! Mama wa watu anaonekana ni ... lakini mzigo alioubeba kwa mwanawe naona ni mzito!!!

    ReplyDelete
  8. Ukiamia kufanya jambo fanya mia kwa mia. sio mguu mmoja ndani mguu mmoja nje! ama kweli ukiyashangaa ya Musa utayaona ya firaini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...