bonde la mbezi ambalo pia ni mpaka wa kawe na mbezi likiwa katika hali ya uchafu.
Maporomoko yanayotokana na mashimo yalimo chimbwa mchanga.
Sehemu ya mrundikano wa taka katika eneo hilo la bonde
Wananchi wasio waadirifu na kujali mazingira wakiendelea na shughuli za uchimbaji mchanga richa ya kukatazwa na mamlaka husika.

Na mwandishi wetu.

Mwandishi wa Globu ya Jamii anaripoti hali tete kutoka katika maeneo ya mpakani mwa mbezi na Kawe inayosababishwa na uchafuzi pia na uharibifua wa mazingira mkubwa unaofanywa na watu wa maeneo hayo bila kujali afya, usalama lakini pia mazingira kwa ujumla.

 Katika eneo hili limekuwepo dampo kubwa lisilo rasmi ambapo kila mkaazi wa eneo hili hutupa taka za aina yoyote ile jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi cha mvua za masika.

Lakini pia wakazi hao wamekuwa wakichimba mchanga kwenye bonde hilo na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa sana wa mazingira jambo ambalo ni hatari kwa majengo yaliyo karibu na bonde hilo.

Pia kuna kundi la vijana katika eneo hili maarufu kama (mateja) kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa nne usiku ambao huchangisha fedha kutoka kwa wananchi kwa madai kuwa wanatengeneza kivuko kwenye bonde hilo na hivyo na kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa wakazi na wapitanjia kwenye eneo hilo. 

Vijana hao wakati mwingine wamekuwa wakipora vitu vya thamani kama simu za mkononi na fedha na hata ripoti zinapopelekwa kwenye vyomba vya dora hakuna hatua zozote za kudhibiti zinazochukuliwa kupambana nao.

Hivyo basi ni rai yetu kwa viongozi husika kwani wanataarifa hizi na wengine hupita hapo na kujionea yanayotokea kuchukua hatua za makusudi ili kunusuru wananchi pia mazingira ya eneo hili.
Habari na picha toka ;http://mkandawilejr.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Unataka tukale wapi? Sisi tumeajiajili wewe unaleta unoko mbona wenye serikali yao (watendaji,wajumbe,madiwani,mkuu wa wilaya,m/mkoa,wabunge,.........)hawajasema lo lolote au unazani hawajui? Acha tuchape kazi bwana, mbona huwa uachi kununua huu mchanga tukikuleta pale unaporomosha mjengo wako wakifsadi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...