Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali na wasanii wa kikundi cha Taarab cha Wanawake,(Tausi Women Musical Club)baada ya kukizindua rasmi ,katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizindua kikundi cha Taarab cha Wanawake,Tausi Taarab wanawake Zanzibar,katika ukumbi wa Salama bwawani Hotel mjini Zanzibar wikiendi hii.
Watoto waliozaliwa katika familia za wanamuziki wa Taarab,Neema Suri,(kulia) na Nabil Mohamed wakionesha vipaji vyao katika fani ya kupiga udi katika uzinduzi wa kikundi cha Wanawake cha Taarab,kiitwacho (Tausi Women Musical Club),uzinduzi wa kikundi hicho umefanywa na Rais wa zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa salama Bwawani Hotel
Wasanii wa kikundi cha (Tausi Women Musical Club) wakicharaza ala ya Muziki wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel.PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...