Spika Makinda (katikati) akiwa na Bw Emmanuel Lupil ambaye ni Mwenyekiti( Kulia0 na Bw. Severini Kapinga Katibu wa Watanzania waishio Korea.
Bw. Lwenje akifafanua jambo.
Kipindi cha maswali na ufafanuzi.
Mtanzania aishiye Korea Kusini mtoto Faith Sanga akitoa zawadi kwa Mhe. Spika kwa niaba ya kundi zima.
Mwendesha shughuli Bi Juliana Masawe akimpongeza Faith na kumshukuru Mhe. Spika kwab kuja kuonana nao.
Picha ya pamoja.Picha zote na Prosper Minja-Bunge.
Wakati wa kuahirisha ziara yake nchini Korea Kusini jana jioni, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda alikutana na watanzaia wanaoishi nchini humo katika Chuo Cha Maendeleo cha Korea (KDI) ambapo waliiomba serikali kupitia kwake (Spika) kutafakari kufungua ubalozi nchini Korea Kusini kwani kuna mengi yatakayoinufaisha Tanzania. Tayari nchi jirani ya Kenya imefungua ubalozi nchini Korea.
Watanzania hao wapatao sitini ambao wengi wao ni wanafunzi wa elimu ya juu walitanabaisha kuwa Korea Kusini ni nchi ambayo ilikuwa maskini sana miaka michache iliyopita lakini imefanya mapinduzi ya kiuchumi na sasa ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea duniani.
“Ni bora kujifunza kutoka kwenye nchi zinazokuwa kwa kasi tukiziona kuliko kutegemea nchi zilizoendelea zamani kama vile za ulaya na Marekani” alisema Bw. Lwenje ambaye ni mwanafunzi wa shada ya uzamili ya uchumi.
Katika risala yao, wameiomba serikali pia itumie vizuri fursa za masomo zilizopo nchini Korea kwa kupeleka wanafunzi wengi zaidi kwa manufaa ya nchi. Aidha waliiomba serika iharakishe mpango wa kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwani ni jambo ambalo kwa sasa hivi halikwepeki tena.
Mhe. Spika akiwaahidi kuyafikisha maombi yao serikalini amewataka kudumisha nidhamu, kufanyakazi kwa bidii na kudumisha uzalendo wa nchi yao.
“Ninyi ndiyo chachu na wakala wa mageuzi mara mtakapomaliza masomo yenu na kurejea nyumbani mkiwa na utaalamu na uzoefu wa yale mtakayokuwa mmejifunza huku” aliwaasa Mhe. Makinda.
Aliwahamisha kuwa hali ya numbani ni shwari ila changamoto ni nyingi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwamba jitihada kubwa zinafanyika kuondoa tatizo la umeme na mchakato wa katiba mpya unaendelea.
Sasa hawa wote ni wanafunzi,Tunataka kuona wanaoishi Korea,kwani Mara ya kwanza hawa wanafunzi ndio walio ogea nae?TUNAITAJI KUONA WATANZANI WOTE,sio kubagua eti WANAFUNZI TU,makina,Jerry,carlos,othumani,bukuku,mzonya,jogoo,frenk,Mose,juma,eriza nk,mpo wapi nyinyi ndio walengwa,hawa wanafunzi wanapita tu,sio wakazi wa kudumu,.
ReplyDeletemchangiaji wa kwanza vipi?kwani kuna mtu aliwazuia hao wakazi wako wasihudhurie?ukiona hivyo ujue wanajificha.
ReplyDeleteUkweli ni kuwa hii ni jumuiya ya Watanzania waishio Korea, sema kuwapata Watanzania wote imekuwa vigumu kwa vile hatuna Ubalozi. Kama ndugu upo hapa Korea jitahidi ujiunge na huu umoja pia wajulishe na wenzako.
ReplyDeletePamoja tutajenga Taifa letu
Wasomi wote mlishindwa kumsaidia huyo mtoto mdogo mzuri katika kuvaa? Mmemwangusha sana, akikua hataipenda hii picha japo ni muhimu na nzuri, kumvalisha mtoto gauni nyeupe na pink then raba za blue na soksi!Vipi mpo hapo?
ReplyDeletewewe unayesema wanajificha kwani wanadaiwa..na hata hivyo mliwatangazia watu wote au mlichaguana wa kuhudhuria hapo kama mdau wa kwanza alivyouliza..ili umoja uwe umoja watu wote washirikishwe na sio kubaguana.
ReplyDeleteJamani tuna lawama amabzo hazijengi,ila zinamong'onyoa.Mama(Spika) amekuja korea,si watu wote ambao walikuwa wakifahamu,imekuwa rahisi kwa wanafunzi kuhudhuria kwa kuwa ni rahisi kwa wanafunzi kufahamu ujio wa spika.Kingine tulitangaziwa kuwa spika ataongea na watanzania ,si wanafunzi tu,wapo baadhi ya watu wanaofanya kazi viwandani,wanaofundisha vyuoni waliohudhuria.Hapo hakuna wa kumshika mwenzake uchawi zaidi ya sisi kwa sisi kutaka kutafuta umaarufu usio na mantiki.Tujenge hoja zenye fikra chanya kabla ya kuziwakilisha mahala husika,watanzania hatupendi ukweli,bali tunapenda sana kulaumu na kunyoosheana vidole .
ReplyDeleteMmh hizi Comment za siku nyingi sana. MIMI NASOMA KOREA SASA-NAWEZAJE KUPATA MAWASILIANO YA UMOJA HUU? Namba yangu ni 01063712343. YEYOTE ANAYEJUA ANIJULISHE TAFADHALI.
ReplyDeleteSASA LIKIZO HIYOO INAANZA. NATAKA KUJIFUNZA KIKOREA. NISAIDIENI NDUGU ZANGU MLIOPO HAPA KOREA
ReplyDelete