Mhe. Bernard Membe, Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitambulisha ujumbe wa mabalozi kwa Mama Maria Nyerere mjane wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, na mtoto wake Makongoro Nyerere walipotembelea nyumbani kwao Butiama. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mabalozi Tanzania Mhe. Balozi Juma Alfani Mpango, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo nchini Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. John Tupa.
Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. K.V. Bhagirath akisalimiana na kumpa zawadi Mama Maria Nyerere alipokuwa kwenye ziara hiyo ya mabalozi Butiama.
Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Alberic Kacou akiangalia baadhi ya picha za Mwalimu Nyerere kwenye Maktaba ya Mwalimu huko Butiama. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule na kulia kwake ni Mkuu wa Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Tim Clarke.
Baadhi ya wajumbe na wanadiplomasia nchini waliokuwa kwenye msafara wakiangalia picha zilizokuwa kwenye maktaba maalumu ya Mwalimu Nyerere Butiama.
Bw. Robert Scort msaidizi wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania akiangalia maonesho mbalimbali kwenye maktaba ya makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kijijini kwake Butiama.
Baadhi ya wajumbe na wanadiplomasia nchini waliokuwa kwenye msafara wakiangalia picha zilizokuwa kwenye maktaba maalumu ya Mwalimu Nyerere Butiama.
Mhe. Balozi Tim Clarke, Balozi wa Umoja wa Ulaya akiangalia picha mbalimbali za Hayati Mwalimu Nyerere alipokuwa kwenye Maktaba iliyohifadhi kumbukumbu za kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania.
Baadhi ya wajumbe na wanadiplomasia nchini waliokuwa kwenye msafara wakiangalia picha zilizokuwa kwenye maktaba maalumu ya Mwalimu Nyerere Butiama.
Mhe. Bernard Membe akifuatana na Mama Maria Nyerere, na viongozi wengine wakiondoka eneo la Kaburi alipozikwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, mara baada ya kuweka mashada na kufanya sala ya pamoja katika eneo hilo. Waziri Membe aliongoza ujumbe wa wanadiplomasia 32 waliopo nchini kutembelea kaburi hilo na kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Ingunn Klepsvik akiwa kwenye Maktaba ya Mwalimu Nyerere kijijini Butiama, akiangalia sanamu ya Mwalimu Nyerere amekumbatia Tanzania. Balozi huyo ni mojawapo ya mabalozi waliotembelea Butiama kumuenzi Baba wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...