Mdadisi wa Sensa ya Majaribio ya watu na Makazi 2011 Bw. Alawi Ally akiendelea na zoezi la kukusanya takwimu za sensa hiyo eneo la Chukwani Zanzibar.
Mdadisi wa Sensa ya Majaribio ya Watu na Makazi 2011 kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzbar Bi.Mwanahawa Yahaya (kulia) akiendelea na zoezi la kuuliza maswali na kujaza fomu za dodoso refu katika eneo la Regeza Mwendo, Chukwani Zanzibar leo.
Wadadisi wa Sensa ya Majaribio ya watu na Makazi ya mwaka 2011 wakiendelea na zoezi la kupita nyumba nyumba hadi nyumba wakiongozwa na mjumbe/sheha wa Shehia ya Regeza Mwendo Bw.Ally Nassoro (katikati) Zanzibar.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Huku Chukwani ndiko wanakohamia watanganyika wengi ili kuongeza idadi za wapiga kura wa CCM. Unamuona dada na kaka wa kibongo hapo juu wanahesabiwa? Wanasubiri 2015 wapige kura.
ReplyDeleteWewe mtoa maoni wa kwanza unahitaji elimu, ni wazi upeo wako ni mdogo, sensa kama hii huwa zinahesabu wakazi halali, hii sio daftari ya wapiga kura wala sio sensa ya Wazanzibari! Hebu jaribu kupeleka nguvu katika kujielimisha.
ReplyDeleteWazo! Serikali fanya sensa kuruhisisha huduma kwa wananchi. Na sio kufanya sensa kutumia gharama kubwa na maendeleo hakuna. Tizima mwenye nyumba kajitahidi lakini inaoneyesha hata umeme hakuna nimeona hadi nyumba nyingine mpaka leo zimmeezekwa makuti japo ni utamuduni lakin soi m ya mwananchi kuishi maisha ya kizaman kila mtu anapenda kuishi kisasa. Miaka hiyo 50 ya Uhuru ni mingi kwa serikali kuahakisha huduma zot muhimu zinapatikana popote na sio mijini pekee kungepunguza msongamano mjini
ReplyDelete