TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE KUTOKA JIJINI MBEYA,INAELEZA KWAMBA KUMEZUKA VURUGU KUBWA SANA JIJINI HUMO KATI YA WAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO AMBAO WANAPANGA BIDHAA ZAO NJE YA SOKO LA MWANJELWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI.
VURUGU HIZO ZIMEZUKA MARA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUANZA KUWAPIGA KWA MAWE MGAMBO WA JIJI WALIOKUWA WAMEFIKA SOKONI HAPO ILI KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA HAO KUFUATIA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MBEYA,MH. ABBAS KANDORO YA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO WALIKUWA WAMEPANGA BIDHAA ZAO BILA MPANGILIO,KIASI KWAMBA HATA BARABARA YA KUPITA MAGARI INAKUWA IMEFUNGWA KUTOKANA NA BIASHARA ZAO.
ASKARI WA JESHI LA POLISI WAMEFIKA KATIKA ENEO HILO MUDA HUU NA KUANZA KUTULIZA GHASIA HIZO HUKU NA WAO WAKIENDELEA KUPIGWA MAWE NA WAFANYA BIASHARA HAO,HALI ILIYOWALAZIMU KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTULIZA GHASIA HIZO.
KUTOKANA NA GHASIA HIZO,HALI IMEKUWA TETE KWA WAKAZI WA MAENEO YA JIRANI NA ENEO HILO LA SOKO NA KUSABABISHA WATU WENGINE KUKIMBIA MAKAZI YAO KWANI WAFANYA BIASHARA HAO WAMEKUWA WAKIANGUSHA MVUA YA MAWE KWA ASKARI HAO,HUKU WAFANYA BIASHARA HAO WAKIWA WAMEANZA KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KUPANGA MAWE BARABARANI.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFATILIA KWA UKARIBU TUKIO HILO NA ITAENDELEA KUWAHABARISHA KADRI MAMBO YATAKAVYOKUWA YAKIENDELEA JIJINI HUMO.
VURUGU HIZO ZIMEZUKA MARA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUANZA KUWAPIGA KWA MAWE MGAMBO WA JIJI WALIOKUWA WAMEFIKA SOKONI HAPO ILI KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA HAO KUFUATIA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MBEYA,MH. ABBAS KANDORO YA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO WALIKUWA WAMEPANGA BIDHAA ZAO BILA MPANGILIO,KIASI KWAMBA HATA BARABARA YA KUPITA MAGARI INAKUWA IMEFUNGWA KUTOKANA NA BIASHARA ZAO.
ASKARI WA JESHI LA POLISI WAMEFIKA KATIKA ENEO HILO MUDA HUU NA KUANZA KUTULIZA GHASIA HIZO HUKU NA WAO WAKIENDELEA KUPIGWA MAWE NA WAFANYA BIASHARA HAO,HALI ILIYOWALAZIMU KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTULIZA GHASIA HIZO.
KUTOKANA NA GHASIA HIZO,HALI IMEKUWA TETE KWA WAKAZI WA MAENEO YA JIRANI NA ENEO HILO LA SOKO NA KUSABABISHA WATU WENGINE KUKIMBIA MAKAZI YAO KWANI WAFANYA BIASHARA HAO WAMEKUWA WAKIANGUSHA MVUA YA MAWE KWA ASKARI HAO,HUKU WAFANYA BIASHARA HAO WAKIWA WAMEANZA KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KUPANGA MAWE BARABARANI.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFATILIA KWA UKARIBU TUKIO HILO NA ITAENDELEA KUWAHABARISHA KADRI MAMBO YATAKAVYOKUWA YAKIENDELEA JIJINI HUMO.
JANA TU HUMU KUNA MDAU KATUWEKEA PICHA YA AKINA MAMA WAKIFANYA BIASHARA BARABARANI MANZES.!!!!
ReplyDeleteDAVID V.
sasa SUGU yuko wapi watu wake wanavunja sheria yeye kajificha wapi? au na yeye yuko kwenye maandamano ya arusha ameacha kuwatumikia wananchi waliomchagua,kweli chadema mna mambo, ukimchunguza huyo mheshimiwa sugu ni kama hajijui kama yeye ni kiongozi wa nini,utakuta muda mwingi anashughulika na mambo ya wasanii tu na kupambana na clouds fm.
ReplyDeleteKama kawaida ya Abbas Kandoro, kila mkoa akienda ataanzisha ghasia na wafanya biashara wadogo wadogo.
ReplyDeleteSi ajabu kuona mkoa wa mbeya unachafuka, sababu ni Kandoro, Dar kulichafuka kila mara wakati akiwa mkuu wa mkoa, kaenda Mwanza kakanyagia kibati kuendeleza vurugu na wafanyabiashara, now it is the same in Mbeya. Wadau msishangae hii ndo style yake ya uongozi. Kutengeneza mazingira ya vurugu ili aonekane kwa aliyemteua. "BILA KUTENGENEZA VURUGU KANDORO HAONEKANI JAMANI"
ReplyDeletewe anon wa pili huna akili
ReplyDeleteMdau wa Fri Nov 11 10:57am 2011.Acha CHUKI wewe.nafikiri hujui unaloliongea.Ki ukweli anachogombania SUGU ni harakati za kukomboa MZIKI wa kizazi kipya BONGO amabao wasanii hawafaidiki isipokuwa wachache wenye uchu wa pesa na wanyonyaji ndio wanaofaidika.Hivyo SUGU kama mbunge ana haki yakuutetea mziki akiwa yeye kama msanii na kufanya kazi yake ya ubunge kama kawaida!!!
ReplyDeleteWe mmwendawazimu hapo juu, Sugu anaingiaje katika vurugu za wamachinga na polisi Mwanjelwa? Ugomvi wa machinga na vyombo vya dola upo mikoa mingi tu, Mwanza, Dar, Moro n.k. Tatizo kubwa katika kadhia ni mipangilio mibovu na kukosa sera mwanana kwa upande serikali yetu katika kutenga maeneo ya kufanyia kazi mbalimbali, sio biashara tu. Tukitatua hili, migogoro ya namna hii itaisha. Tusiangalie tulipoangukia, tuangalie tulipojikwaa. Sera zetu nyingi ni mbovu.
ReplyDeleteAbbas Kandoro alivyokuwa jiji la Mwanza alikuwa analeta vurugu kwa wamachinga, tangu ameondoka mambo yamekuwa shwari, sasa amehamia Jiji la Mbeya vurugu kazianzisha.
ReplyDeleteNapo mtakurupuka nakusema CHADEMA wakati raia wanaonewa masoko mnachoma wenyewe halmashauri tunajua kabisa hujuma zenu. Mpaka sasa wamekufa watu 3. JK nchi imekushinda hii haitawaliki na huko udsm nako kumenuka
ReplyDeletehyo jamaa aliyeandika kuhusiana na sugu kweli kilaza,hata matatizo ya kimsingi katika jamii mnataka ushabiki wa kisiasa?tuna miaka mingi ijayo kufikia uelewa wa kiwango unachoweza kusema ni cha kuridhisha.
ReplyDeleteKandoro chapa kazi, tunakutegemea. Uliishafisha Kariakoo, ingawaje sasa inaanza kuelekea tulikotoka. Maana baada ya kwako waliofuatia wanafanya kazi kihuruma badala ya kufuata taratibu! BIG UP!
ReplyDeleteSerikali itafute njia ya busara ya kuendesha utawala dhidi ya ''Grassroot Pedlers'' (yaani wafanya biashara ndogo ndogo).
ReplyDeleteNchi nyingi zilizopiga hatua kimaendeleo zime zingatia sana SME (Small Medium Enterprises) na watu kama hawa Machinga ,,,huku tukitambua kuwa AJIRA ni tatizo kubwa kwa nchi nyingi Duniani ikiwemo Tanzania.
We mke wa mtu nini mambo ya sugu na clouds fm yameingiaje humu ya mbeya mwachie kandoro na sugu amwachie sugu shoga nini ww
ReplyDeletewewe Anonymous wa 2 una utaahira au umetumwa!?
ReplyDeleteHujui kama watu wapo bungeni?
Wakuu wa nchi inabidi kuwa macho na haya machafuko ya hapa na pale yanayojitokeza historia inatuambia kwamba mambo yanaanza madogo baadaye huya yanalipuka kila kona ya nchi, uingereza yalianza hivi hivi na nchi nyingine kama Egypt n.k
ReplyDeleteViongozi msidharau hali hizi!
Sasa Mbeya si vurugu za wamachinga tena bali ni vurugu za kisiasa kati ya utawala na upinzani. tunaishukuru sana blog hii kwa kutupatia habari mapeeema kabisa!!!
ReplyDeleteFUNGO B.
MBEYA.
Kandoro Hana lingine Ila Hilo, Hana njia mbadala Kweli mpaka nguvu??
ReplyDeleteLazima aangalie alternative , mwanza kaleta matatizo na Mbeya tena..!!!
Huyo anasema Sugu hivi anataka naye aingie road? Upeo Mdogo acha kuongelea mada usizoweza
wewe mdau waa pili una chuki na chadema na sugu.Sugu yuko wapi kwani hujui kuwa bunge limeanza.wewe hata jambo dogo hilo hulijui au unakurupuka tu.jipange kabla ya kuropoka
ReplyDeleteMasikini Watanzania! Tatizo kila kitu ni siasa. Vurugu kama hizo ni zakiutendaji Sugu wa watu wala hahusiki. Viongozi wetu mipango mikakati yenu ni mibovuuuu na ndio chanzo cha matatizo yote. mfano leo bungeni mnataka pitisha ununuzi wa mali za uma zilizotumika,! .. mnaandaa vurugu pale mtakapo tununulia scraper........ JK amka.
ReplyDeleteJK angalia uongozi wa Kandoro tafadhali na ufanye maamuzi magumu wewe kama raisi, haiwezekani kila mkoa anaoenda kuwa mkuu wa mkoa aanzishe vurugu na wafanya biashara ndogo ndogo, mbona tangu ametoka mwanza au pamekuwa shwari, na mbona kwenye mikoa ambayo yeye hajawahi kutawala vurugu za aina hii hazijawahi kutokea? Kutumia nguvu au kutumia Jeshi sio suluhisho hata siku moja kwenye nchi ya kidemokrasia.
ReplyDeleteNikweli mtupu wakuamka sio JK pekeyake, safu ya watendaji wake pia wamelala.kwanini wasiwe na mipango endelevuuu? ambayo itafanyakazi hata kwamiaka kumi au zaidi. haowamachinga wagepatiwa maeneo mapema ni lini wangejipanga barabarani? nilini vurugu kama hizi zingetokea? mfano kariakoo gorofa wanaloishi polisi pana vinyesi na harufu mbaya sana, inaonyesha wazi miundombinu ya majimachafu imezidiwa, chakushangaza magorofa yanazidikujengwa kwa kasi ya ajabu achilia mbali ubora wa magorofa hayo. nauliza wafanyabiashara wa kariakoo wakiamua kwa pamoja kuchoshwa na harufu mbaya za vinyesi na mikojo mtasema wametumwa na mbunge wao?
ReplyDeleteILI TANZANIA IENDELEE TUTENGANISHE SIASA NA TAALUMA ZA WATU. lasivyo tutabaki kumtafuta mchawi.
Wewe unaye uliza sugu yko wapi nakushanga sana unaonyesha ni jinsi gani ulivyo na upeomdogo. Vurugu chuo kikuu cha dar zina mhusu sugu? Vuru Udom zinamhusu sugu? wananchi wanoporwa ardhi zao shinyanga ili kupisha mwekezaji wa madini zina mhusu sugu? vurugu za dowansi zinamhusu sugu? mfumuko wa bei unamhusu sugu? kuporomoka kwa shilingi kuna mhusu sugu? haya sasa nimeona kuna mchangiaji ansema serikali inataka ianze kununua vitu used, outcome yake atakua ni sugu? acha ushamba wewe watanzania wamechoka.
ReplyDeleteRizwani uliambiwa ongea na mshua! street kimenuka, ujumbe ulifikaa? hizi vurugu kila kukicha sio ishara nzuri, inaonyesha wazi watanzania wamechoka...........
ReplyDeleteJK. Kandoro nimuwajibikaji hatukatai. ila asionee vidagaa kuna ukoloni wa kisasa kupitia uwekezaji wa mikataba mibovu apambane nao ili kunusuru nchi yetu na watanzania wengi wafaidike na madini yao wanayoyafaidi wachache. sio kupambana na wamachinga kila mkoa anaokwenda.