Na Gladness Mushi - Arusha
Mwili wa mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni dereva wa bodaboda, ambaye hakutambulika kwa haraka,umekutwa umetelekezwa kandokando ya Mto kwenye shamba la migomba, ukiwa na majeraha kichwani na macho yakiwa yamenyofolewa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha ,Akili Mpwapwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema tukio la kukutwa kwa mwili huo limetokea novemba 8 mwaka huu majira ya saa12 jioni katika mtaa wa jamuhuri daraja mbili katika manispaa ya Arusha.
Alisema kuwa marehemu alikutwa katika shamba la migomba ambalo linamilikiwa na Richard Laiza ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo.
Alifafanua kuwa Laize ndiye aliyeuona mwili huo na kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa huo Husseini Dudu,ambaye baada ya kushuhudia tukio hilo aliyoa taarifa polisi.
Aidha uchunguzi wa awali wa polisi ulionyesha kwamba marehemu alipigwa na kitu kizito na chenye ncha kali kichwani na kisha kutelekezwa katika shamba hilo.
Hata hivyo kwa kuwa mwili huo ulibainika kuharibika vibaya na uchunguzi wa daktari ulifanyika eneo hilo la tukio na mwili wa marehemu ulizikwa katika shamba hilo baada ya kutofahamika ndugu wa marahamu huyo.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wa mauaji hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...