Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Asante sana wana blog..picha nzuri sana.Hawa walikuwa hawana mchezo..ndiyo maana mwaka 1985(nikiwa mdogo) dola moja ilikuwa sawa na sh.6 hivi za Tanzania(sina uhakika)..nakumbuka senti hamsini ile yenye kisungura tulikuwa tunajichana na pipi zile za vidonge hadi basi..tumetoka mbali.

    David V

    ReplyDelete
  2. Dah! Wamependeza sana na hizo suti zao. Hapa walikuwa bado hawajaanza kuvaa zile Chou En-lai ambazo zilikuwa zinanikera kupindukia.

    ReplyDelete
  3. Sawa sawa, kikosi kimetimia!!!...picha hii ni hazina kubwa!

    ReplyDelete
  4. Kikosi kazi No Ufisadi, No Ubinafsi, No Mgao, No $$ Transactions, No Vitambi,No albino Killings, Shule zote mpaka chuo kikuu, kula,kulala huko Bureeee, Hospitali dawa bure(hakuna kwenda India), Kazi zipo viwanda vinafanya kazi, Kila mtanzania alikuwa mzalendo, kwa sasa tunahitaji rehema za MUNGU nchi haina wenyewe, MUNGU TUSAIDIE!!!

    ReplyDelete
  5. Yeah hapa ilikuwa kabla Nyerere hajaenda China na kurudi na experiment ya Ujamaa. Ujamaa umeilostisha TZ na legacy ya Mwalimu.

    Long Live Free Market Capitalism!

    ReplyDelete
  6. wewe hapo mwaka 1986 dola moja haikuwa sh.6 ilikuwa imeishafika sh.500kwa dola1

    ReplyDelete
  7. Anonymous wa kwanza, mwaka 1978 dola moja ilikuwa sawa na Sh. 7 na Pauni ya kiingereza Sh. 20. Mwaka 1985 ilikuwa kwenye Sh. 13. Dola ilianza kuporomoka pale tuliposema hatuangalii nyuma tusijegeuka jiwe (Mzee Mtei anaikumbuka vizuri hii).

    Anonymous wa nne hiyo bureeee ndiyo iliyotufikisha hapa. Mwaka 1964 Azimio la Arusha ilikuwa bado kwa hivyo wenye viwanda halisi ndiyo waliokuwa wakiviendesha.

    ReplyDelete
  8. Long Live Free Market Capitalism Sio. Kwa nini mnalia "ufisadi" umekithiri? Kila siku tunasikia mnalia kuwa jamaa ni milionea kaiba pesa sijui kafanya hivi na vile. kwa nini msimwache aendelee kuwanyonya?

    ReplyDelete
  9. picha tu inaonesha full integrity!

    ReplyDelete
  10. hahahaha kweli mbona hawana vitambi?????? naona vilikuwa haviruhusiwi na ilikuwa sheria labda. Mamamamama sasa Nyerere ingeewezakana ukaja Ofisi wote Vitambi baba , hata wanawake,wapejikoboa hao ka wazungu

    ReplyDelete
  11. Mdau David V kweli mwaka 1985 ulikuwa mdogo sana. Nadhani bado ulikuwa chekechea (enzi hizo zillitwa shule za vidudu). Mwaka huo dola moja ilikuwa ni tayari zaidi ya shilingi 200. Au unamaanisha mwaka 1965?

    ReplyDelete
  12. Mimi naomba kuuliza nini kimetokea kwa nchi yetu???? Mbona imepoteza kabisa mwelekeo?

    Mwezi uliopita nilikuwa Dar. ni bora kukaa kijijini kuliko Dar, hakuna maji,umeme, barabara ndo kwanza haziendi, kila bei kuubwa sana.

    Sioni haibu kusema kwamba, roho yangu ililia kabisa kuona tumeshindwa kujikwamua

    ReplyDelete
  13. Lakini wachina waliomfundisha Mwalimu Ujamaa mbona wanasonga mbele kiasi kwamba wamarekani hivi sasa wanahofia maendeleo ya mchina na jinsi anavyochukua dunia kwa kasi ya ajabu ( new super power in the making). Sasa swali linakuja kwamba tatizo ni ujamaa au watanzania wenyewe? Sasa hivi wachina wameamua kuja kabisa mpaka manzese na wanazidi kuendelea hapo hapo nyumbani kwenu na sisi wana-wa-majungu uvivu mbele tunapiga kelele ujamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!????????????????????????????????????????????? Maswali mengi. Kumbuka enzi za Mwalimu mafisadi kulikuwa hakuna...Kesi za uhujumu uchumi kila kona. What went wrong???

    BABU YENU
    MZEE WA BUSARA

    ReplyDelete
  14. mKIambiwa Mwalimu alikuwa mdini mnakataa. Baraza zima Muislamu Mmoja. Kweli waislamu wengi walikuwa hawajasoma lakini wale wa wachache wakuokota okota walikuwapo. ukweli ni kwamba Mzee huyu alikuwa anavaa kibalagashia ili kuwalaghai waislamu kama ndugu yao huku anawalima kimya kimya kimya kwa staili ya panya..puliza ng`ata.

    ReplyDelete
  15. ukikaa unakunja 4!!

    ReplyDelete
  16. Hii picha chiboko! Wengine wataiona kama sumu. Shauri yao.
    Binafsi yangu mavazi sio kitu, lakini kazi nzuri saana waliifanya. Hawa ndiyo waliotufundisha waTZ kuwa na utu, ndiyo waliolisogeza Taifa mbele hata kuwa na kitu cha kumuonyesha mkoloni baada ya miaka kumi ya uhuru. Poleni Waheshimiwa kwa kazi.
    Wale walioko bado hai ninapenda kuwapongeza sana. Na wale waliotutangulia Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa Amani.

    ReplyDelete
  17. Tanzania takwimu za jando kwa wanaume zinaweza kutupatia ukweli kuhusu wale wanaoamini ktk dini za asili, kizungu (kikristo) na kiarabu (Kiislamu).

    Kwa Tanzania idadi kubwa ya wakristo wanaume wametiwa jando, kwa waislamu asilimia 100 wametiwa jando na kwa wale waaminio dini zingine mbali na ukristo/uislamu asilimia kubwa hawajatiwa jando.

    Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 40% tu ya wanaume wa tanzania wametiwa jado, hivyo basi Uilslamu hauwezi kuwa dini kubwa kufikia asilimia 30 % ya Watanzania.

    Mtafiti wa jando.
    Ngariba

    ReplyDelete
  18. Mdau umekosa la kuandika. Kukaa na kuandika nne sio dhambi.Wala negative body language, hasa kwa wakati huo na ukizingatia kuwa hawa watu ni kina nani. Inaonekana una kachuki ka kijinga tu. Kama alivyosema mdau hapo juu kabla yako kuwa wengine wataiona hii picha kama sumu kwao. Inawezakana wewe ni mtoto wa fisadi au ni fisadi mwenyewe. Pole sana.

    ReplyDelete
  19. Msitudaganye 1985 dola haikuwa Tshs 500. Nakumbuka dhahiri miaka ya 1994-1995 ndo dola ilikuwa inabadilishwa kwa Tsh 500.Kama dola ingekuwa inabadilishwa kwa shs 500 mwaka 1985 basi sasa hivi tungekuwa tunabadilisha kwa shs 3000-4000. Nasema hivi sababu nilibadilisha dola kibao enzi hizo.Dingi alikuwa ananituma nikabadilishe pesa wakati niko form 1.Sababu Mwanafunzi ni less suspected kukabwa mitaani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...