Kuna wadudu wengi wanaotuzunguka, wengine tunaishi nao majumbani hata kama hatuwapendi. 


Inzi (housefly or scientifically musca domestica), ni mdudu wa kawaida kabisa kwa wengi wetu mwenye madhara mengi kuliko faida kwa mwanadamu. 


Wengi  hatujakaa tukajifunza angalau kidogo kuhusu mdudu huyu. Leo naomba nikuhabarishe kidogo tu kuhusu jamaa huyu “mtoto wa nyumbani” ambaye twafahamu hasikii hata kama ukimfukuza vipi atapenda kurudi na kutua sehemu ambazo wengi hatupendi.
 Inzi hana meno hivyo hula chakula cha majimaji tu ambacho ni pamoja na kinyesi (feces), vitu vilivyooza (moist, decaying organic matters), vidonda (open sores), na vitu vingine vilivyoharibika na kuoza.
 Inzi ana ulimi ulio kama mrija ambao huutumia kufyoza chakula chake. Akiona chakula kigumu, hukitemea mate au kukitapikia ili kilainike kisha hukifyonza. Inzi hucheua chakula kisicholainika sawasawa na baadaye kukila tena kikishalainika. 
Inzi ana mabawa mawili na miguu sita ambayo pia huitumia kuonjea chakula. Miguu ya nzi ina uwezo wa kuonja sukari mara milioni 10 haraka zaidi ya ulimi wa mwanadamu!!. Inzi hutumia milingoti (antenae) yake kunusia.  Ingawa inzi ana lensi 4000 ndani ya macho yake, lakini huona vizuri umbali wa inchi 24 hadi 36.
Sehemu nzuri za inzi kutagia mayai ni zenye unyevunyevu mchafu, wenye joto na vitu vilivyooza kama vyooni hasa vya shimo, jalalani, n.k. Mama inzi mmoja mwenye afya nzuri anaweza kutaga mayai 50 mpaka 75 kwa mtago mmoja hadi mayai 500 – 1000 kwa maisha yake yote. 
Kukupa tu wazo jinsi inzi wanavyoongezeka kwa haraka, kulingana na hekima za mtaalamu wa wadudu  (entomologist) mmoja aitwaye Hodges: wakiwepo inzi wawili (baba na mama) wenye afya nzuri, wakianza kazi Aprili; ifikapo Augosti, inzi hawa watakuwa wametengeneza jeshi la inzi wengine wapatao 191, 010, 000, 000, 000, 000, 000!!!. Hebu Angalia inzi wakifanya vitu vyao hapa: http://www.arkive.org/house-fly/musca-domestica/video-09a.html

Vijichanga vya inzi au viwavi (larvae or maggots) ni vyeupe ambayo hubadilika kiukuaji (pupate) na kuwa inzi kamili, ambaye huweza kuishi (lifespan: hatch to dispatch) kwa wiki mbili hadi mwezi mmoja kulingana na mazingira. Inzi hupitia metamorphosis (mtafsiri tafadhali) na maisha kamili ya aina nne (lifecycles – progress from egg to actual housefly) yaani kama yai (egg), larva or maggot, pupa na kisha inzi kamili. Yai hukaa hadi siku moja na kuanguliwa kuwa kiwavi; kiwavi hukaa hadi wiki moja na kubadilika kuwa inzi kamili.
Wataalamu wanadai kuwa kuna zaidi ya aina 87, 000 za inzi (sio wa nyumbani tu) duniani; lakini inzi wa nyumbani (housefly) ninayewazungumzia hapa ndiwe wengi, karibu asilimia 91 ya nzi wote wanaoishi mazingira ya wanadamu (domestic).  
Inzi si mdudu mzuri kama tunavyojua na tulivyoona awali kwa sababu ni mleta magonjwa mengi yanayotesa duniani kote. Baadhi ya magonjwa yanayosabishwa na inzi (samahani mengine siyafahamu kwa Kiswahili – anayeweza atanisaidia) ni pamoja na homa ya typhoid, homa ya manjano (yellow fever),  kifua kikuu (tuberculosis), ukoma (leprosy), kipindupindu (cholera), kuharisha (diarrhoea), minyoo (parasitic worms), dysentry, anthrax, bubonic plague, scalet fever, yn.k. 
Inzi wanaweza kubeba chembe chembe zinazoweza kusababisha magonjwa (disease causing microorganisms) ndani na nje ya miili yao. Inzi mmoja anaweza kubeba hadi chembe chembe milioni mbili na hivyo kuwa sababu ya magonjwa ya mlipuko. Ukimwona ametua kwenye mkono wako au kwenye kikombe chako cha chai, anaweza kuwa kaacha mamilioni ya chembe zinazoweza kukupa maradhi ya kutisha; inzi ni hatari kwa afya yako na familia yako.
Ingawa inzi ni kati ya wadudu wanaoruka upesi sana (4½ mph), mara nyingi hawasafiri mbali na walikozaliwa, ingawa upepo unaweza kuwabeba mbali. Inzi hupenda sana harufu mbaya na mazingira machafu; hivyo ukitaka wakutembelee, harufu mbaya ni kadi mojawapo nzuri ya kuwaalika.
Pamoja na hasara zote hizo nilizotaja, wengi wetu tutashangaa kusikia kwamba inzi wana faida ya moja kwa moja kwa mwanadamu katika nyanja ya matibabu!!.
 Madaktari katika nchi za wenzetu wamefanikiwa kutumia aina ya viwavi (a special species of maggots) kuwasaidia wagonjwa wenye vidonda vibichi hasa vidonda vilivyosababishwa na kuungua moto. 
Viwavi huachiliwa kwenye vidonda na kula nyama ya sehemu iliyoungua, iliyoharibika ambayo husababisha donda kupona.  Ingia hapa uone inzi aliyevishwa ‘cool shades’ mambo ya majuu haya – salale!!! http://news.nationalgeographic.com/news/2006/03/0328_060328_fly_glasses.html
Siku nyingine usishangae daktari atakapofunua moja ya kabati lake na kuachilia hawa jamaa wakusaidie kwenye donda, wala hutahitaji kwenda kwenye duka la dawa; pengine liwe duka linalouza hao jamaa!!.

Mwandishi Damas anapatikana kupitia bdmas2004@hotmail.com. Kama habari hii imekusaidia, mtumie ujumbe tu wa kumtia moyo ili aendelee kuhabarisha umma. Ujumbe umekusanywa kutoka sehemu mbalimbali za tovuti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hongera kwa ku2habarisha... tunaomba uzidi ku2habarisha zaidi na zaidi.. haya ni masuala muhimu sana.

    ReplyDelete
  2. Huyo haitwi INZI kama ulivyoandika bali anaitwa "NNZI" huandikwa tu "NZI", ndiyo pichani pichani, huyo unayesema wewe INZI hatumjui au hilo neno halipo katika kiswahili fasaha, kama ilivyo katika kiingereza, kunamaneno yanaandikwa tofauti na yanavyosemwa ndivyo ilivyo na ni sahihi, kwa mfano katika kingereza kunaneno "WEDNESDAY" Linatamkwa "wensday" unaona tofauti kabisa na linavyoandikwa, ndivyo ilivyo kwa neno "NZI" Linatamkwa "nnzi"

    ReplyDelete
  3. Kumbe pamoja na balaa zote zilizoorodheshwa katika kukusanya magonjwa naye ana faida zake!! Asante kwa kutuhabarisha, tafadhali endelea kutuelimisha kila upatapo ya kuelimisha.

    Ankel, hii ndiyo faida ya mtandao huu wa jamii, ubarikiwe ankel na mtoa mada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...