Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Halima Dendego,( wapili kutoka kulia) akiwakabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi wawili walenzi na viongozi wa wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga, katika Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni mkono wa sikukuu ya Idd El Hajji. Wa kwanza kulia ni Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa , Bw. Oswin Ngungamtitu.
Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Ahmed Ng’eni ( kulia) akisaidiana na mmoja wa vijana wanaoishi karibu na Kambi ya Funga Funga iliyipo Manispaa ya Morogoro ambayo wanaishi Wazee wasiojiweza ,kurejesha mbuzi aliyekata kamba na kukimbia , kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima Dendego ( hayupo pichani) ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, wakati wa kutoa zawadi ya vyakula na mbuzi kama zawadi toka kwa Rais Jakaya Kikwete kama mkono wa sikukuu ya Idd El Hajji.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Halima Dendego akimkabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi Mwenyekiti wa Kambi ya wazee wasiojiweza ya Funga Funga, katika Manispaa ya Morogoro, Joseph Kanika toka kwa Rais Jakaya Kikwete. Wa kwanza kushoto) ni Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa , Ahmed Ng’eni.
Picha zote na mdau John Nditi
Kiongozi, huyo mbuzi mlivyombeba ni sawa? AU kwa sababu mtamchinja hivyo haina tofauti?
ReplyDeleteSi sawa hata kama atachinjwa..Wamembeba vibaya sana huyo Mbuzi, picha ya katikati..huyu Mkuu ndiye yule Halima Kihemba au?
ReplyDeleteHeshima kwa wanyama tafadhali.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu hapendi dhuluma ya aina yeyote dhidi ya viumbe wake. Watendeeni wema, kwa ubinaadamu na pia kuepuka adhabu zake.
ReplyDelete