Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Halima Dendego,( wapili kutoka kulia) akiwakabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi wawili walenzi na viongozi wa wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga, katika Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni mkono wa sikukuu ya Idd El Hajji. Wa kwanza kulia ni Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa , Bw. Oswin Ngungamtitu.
 Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Ahmed Ng’eni ( kulia) akisaidiana na mmoja wa vijana wanaoishi karibu na Kambi ya Funga Funga iliyipo Manispaa ya Morogoro ambayo wanaishi  Wazee wasiojiweza ,kurejesha mbuzi aliyekata kamba na kukimbia , kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima Dendego ( hayupo pichani) ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, wakati wa kutoa zawadi ya vyakula na mbuzi kama zawadi toka kwa  Rais Jakaya Kikwete kama  mkono wa sikukuu ya Idd El Hajji.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Halima Dendego akimkabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi Mwenyekiti wa Kambi ya wazee wasiojiweza ya Funga Funga, katika Manispaa ya Morogoro, Joseph Kanika toka kwa Rais Jakaya Kikwete. Wa kwanza kushoto) ni Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa , Ahmed Ng’eni. 
Picha zote na mdau John Nditi  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kiongozi, huyo mbuzi mlivyombeba ni sawa? AU kwa sababu mtamchinja hivyo haina tofauti?

    ReplyDelete
  2. Si sawa hata kama atachinjwa..Wamembeba vibaya sana huyo Mbuzi, picha ya katikati..huyu Mkuu ndiye yule Halima Kihemba au?

    ReplyDelete
  3. Heshima kwa wanyama tafadhali.

    ReplyDelete
  4. Mwenyezi Mungu hapendi dhuluma ya aina yeyote dhidi ya viumbe wake. Watendeeni wema, kwa ubinaadamu na pia kuepuka adhabu zake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...