Mh. Mohammed Dewji akionyesha karatasi zenye hundi aliyokabidhiwa leo ofisini kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni za GURJAR GRAVURES  na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED za nchini India Bw. Zainuddin Mahuwala (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) hundi ya $ 15,000/= kwa ajili ya kusaidia jitihada zake za kuboresha Maendeleo katika jimbo lake la Singida Mjini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hizo Bw. Shubair Mahuwala.

Na.Mwandishi wetu.

Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji leo amepokea jumla ya dola za kimarekani elfu 15 kutoka kwa kampuni ya GURJAR ya India kutokana na mchango wake katika kutoa huduma  kwa jamii hususan kuwasaidia yatima na watoto ambao wazazi wao hawana uwezo.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa na kampuni mbili zinazomilikiwa na Zainuddin R. Mahuwala za GURJAR GRAVURES PRIVATE LIMITED ambayo imetoa dola 7,500 na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED ambayo imetoa dola 7,500.

Akipokea hundi ya fedha hizo Mh. Dewji amesema atazielekeza katika mfuko wa huduma za elimu wa Mohammed Foundation ambao umekuwa ukisaidia kuwasomesha watoto zaidi ya 2400 katika jimbo la Singida Mjini.

Wakati wa makabidhiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ofisini kwa Mh. Dewji, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hizo Bw. Zainuddin Mahuwala ambaye aliambatana na mtoto wake Shubair Z. Mahuwala ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hizo, amempongeza sana mbunge huyo na kumtaka kuendelea na moyo huo wa kusaidia jamii huku akimuombea Mungu amzidishie.

Mh. Dewji amekuwa akipigania kupatikana kwa fursa sawa ya elimu kwa watoto Singida mjini ikiwemo kujitolea kukarabati na kujenga shule sambamba na kununua vifaa vya elimu. Kwa sasa Mh. Dewji anasomesha watoto zaidi ya 2400 yatima na ambao wazazi wao hawana uwezo ili nao wapate nafasi ya kupata elimu itakayowasaidia kujikomboa katika maisha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hongera na asante sana MO kwa juhudi zako na kazi yako nzuri kuwapunguzia watu wa jimbo lako shida.

    ReplyDelete
  2. jazzakal lahu khair inshaallah...ni mwanzo mzuri tu wa safari ndefu MO...nimefarijika kwa hilo, sana tu maana mi niwe mkweli tu, ni mwenyeji wa huko lakn ni cngda ya kusini jimbo la msanga.,.Hongera na mungu akuongoze ktk hayo yote

    ReplyDelete
  3. Pamoja na hilo hawa jamaa watakuwa wamalipa fadhila fulani!Hakikisheni baada ya hapo baba na mwana wanarudi kwao...hawakawii kuhamia hasa hapo Singida kwenya dhahabu....!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...