Doreen Estazia (kulia) akiwa na baadhi ya madesign nchini Afrika Kusini alipokwenda kupata uzoefu wa Afrika Fashion Week baada ya kualikwa na Millen Magese (Happiness Magese). Mbunifu huyo amepania kuiwakilisha Tanzania kimataifa.
Doreen Estazia (kulia) akiwa na baadhi ya madesign nchini Afrika Kusini alipokwenda kupata uzoefu wa Afrika Fashion Week baada ya kualikwa na Millen Magese (Happiness Magese). Mbunifu huyo amepania kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Na Mwandishi Wetu

MBUNIFU wa mitindo nchini, Doreen Estazia amesema kuwa malengo yake makubwa ni kuwa mbunifu wa kimataifa mbali ya kushika namba moja hapa nchini.

Estazia amesema hayo jana wakati akiwa anazungumzia mipango yake ya baadaye katika masuala ya maonyesho ya mavazi na ubunifu hapa nchini.

Alisema kuwa ameanza kupata uzoefu wa kimataifa baada ya kushuhudhia maonyesho makubwa kabisa ya ubunifu wa mavazi Afrika yajulikanayo kwa jina la Africa Fashion Week yaliyofanyika Afrika Kusini.

Alifafanua kuwa yeye alipelekwa huko na mwanamitido anayetesa katika anga za kimatafa, Millen Magese (Happiness Magese) ambaye ndiye alimwalika na kuwa miongoni mwa wabunifu waliofungua macho katika sekta hiyo.

“Nampongeza sana Millen kwa kunipa sapoti kubwa kwa kunipeleka huko na kupata uzoefu mkubwa, nimepata mwanga na nguvu mpya kwani lengo langu kubwa ni kushiriki katika Maonyesho ya Mavazi ya Afrika ambayo Magese ana jina kubwa sana huko,” alisema Estazia.

Alisema kuwa malengo yake makubwa pia ni kufanya vizuri katika Swahili Fashion Week (SFW) na anaomba mashabiki kumpigia kura kwa kuandika UCD Eskado Bird kwenda namba 15678.

Mbali kwa njia ya meseji, pia mashabiki wanaweza kupiga kura kwa kuandika , Eskado Bird kwa mwaka 2011 kupitia mtandao, http://www.swahilifashionweek.com na vile vile kutembelea au kufungua mtandao wake, Eskado Bird fan katika Facebook au www.eskadobird.com kuweka ‘clip’.

Estazia pia anatarajia kuzindua staili mpya ya viwalo ijulikanayo kwa jina la What’s Your Freedom (WYF) katika Swahili Fashion Week (SFW) chini ya lebo yake, Estado Bird na viwalo hivyo ni moja ya kuadhimisha sherehe ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

Alisema kuwa ameamua kubuni nguo hizo ili kutoa fursa kwa kila mvaaji awe huru na chaguo lake. Alisema kuwa nguo hizo zimetengenezwa malighafi ya hali ya juu na hali kadhalika ubora wake ni wa kipekee kabisa.

“Nimetengeneza nguo za jinsi zote tofauti na mawazo ya wengi, kuna nguo za kike za kila ana na vile vile kuna nguo za kiume, nataka kuonyesha kuwa nami ni miongoni mwa wabunifu bora katika fani hii,” alisema Estazia.

Alifafanua kuwa mbali ya kushiriki katika Swahili Fashion Week, pia amewaomba mashabiki wa masuala mavazi nchini kumpigia kura katika maonyesho hayo ya kila mwaka ili aweze kushinda katika kinyang’anyiro cha mbunifu anayekuja juu kwa kasi.

Alisema kuwa kula zinatakiwa kupigwa kwa kuandika lebo yake, Eskado Bird kwa mwaka 2011 kupitia mtandao, http://www.swahilifashionweek.com na vile vile kutembelea au kufungua mtandao wake, Eskado Bird fan katika Facebook au www.eskadobird.com kuweka ‘clip’.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. anko swalama?
    mie nipo paje unguja.
    nipatie mawasiliano ya huyo kushoto.
    kwa ihsani yako ankal au wadau kama wana mawasiliano yake. plis plis plis

    ReplyDelete
  2. sasa hata kazi zake hatujaziona, anaomba 'kula'.

    ReplyDelete
  3. Wewe wa Paje Unguja unaeomba kwa Ankal mawasialiano na wa huyo wa kushoto...TANZANIA TUMEKATAA isije ukawa unazipitisha SERA ZA MSAADA WA WAINGEREZA alizotoa Donald Cameron!

    ReplyDelete
  4. Wewe anony wa Tue.Nov 08, 04:33;00PM
    Tanzania imekataa?? Na huyo wa kushoto ni nini? Jamani ni kheli tukubari tu, maana tutapoteza vyote, maadili mema na misaada pia. Kwa mtaji huu hapo juu tumeshapoteza maadili, ni kheli tuambulie misaada.

    ReplyDelete
  5. HAHAHAH wewe Anonymous wa Wed Nov 09, 07:17 AM 2011 sasa msaada huo utafaa nini wakati tushakuwa MABWABWA kupoteza kimoja kama hapo juu , ni bora tukose cha pili ili turekebishe hali ya hewa,Bora uone inatokea kwa wengine, MAANA AIBU HIO USIOMBE IWE NDANI YA UKOO WAKO INAUMA SANA MUHUSIKA UNAHESHIMIKA LAKINI MWANAO WA KIUME ANA MUME!,
    -----------------------------------
    Unakuta sometimes ukitoka jamaa wanakuja wanamzengea mwanao KIJANA WA KIUME na wanamgongea nyumbani kwako! kulaleki!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...