Golikipa wa timu ya taifa ya Chad, Brice Mabaya akirukja kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake mbele mshambuliaji wa Taifa stars katika mchezo wa kutafuta nafasi za kufuzu katika mchezo wa kuwania kutinga katika hatua ya makundi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Chad ilishinda 1-0.
 Kocha wa Taifa Stars Jean Poulsen 'Babu' akiagana na kocha msaidizi wa Chad baada ya kumalizika kwa mchezo
 Mashabiki wakifuatilia mchezo huo
 Nahodha wa Stars Henry Joseph (shoto) na nahodha wa Chad, Mahmat Habib kabla ya mchezo
Wachezaji wa Chadi wakiagana na wenzao wa Stars baada ya mchezo kwisha
 Juu na chini ni mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mrisho Ngasa (shoto) akichuana na beki wa Chad, Rodrigue Casmir Niinga katika mchezo wa kutafuta nafasi za kufuzu katika mchezo wa kuwania kutinga katika hatua ya makundi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Chad ilishinda 1-0. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Kwenye makundi inabidi watafute namna ya kushinda. Ama Polusen abadili mbinu, ama Maximo arudishwe, au kocha mpya mwenye kuzijua vizuri Ivory Coast na Morocco atafutwe.

    ReplyDelete
  2. MAXIMO BORA KULIKO "BABU" ILA MAONI YANGU NAONA NI HIVI SI MAFUNDI WENYE KUIJUWA IVORY COAST WALA MOROCCO HIZO TIMU MBILI ZINAJULIKANA NA WENGI TU KWA KUZITIZAMA NA KUJUWA MBINU ZAO WAO NDIO HAWATUJUI SIE SANA NI KUTOWA UOGA NA KUCHEZA KWA KUJIAMINI NA KUJIFUNZA MAKOSA MENGI KWA IVORY COAST TULIVYOCHEZA NAO NA HASA MOROCCO KILA LA KHERI TAIFA STARS. MZ

    ReplyDelete
  3. Wewe namba moja umeninyang'anya tonge mdomoni.TFF kaeni chini na wadau jamani, mwezi wa sita 2012 siyo mbali.Mambo ya kujadili ni pamoja na haya hapa.

    1;Je mbinu zinazotumiwa na timu ya Taifa zinafaa kwenye michuano hii?

    2;Je timu hii inaweza kuhimili vishindo vya Gambia,Morocco na Ivory coast?Je Ni timu sahihi au ibadilishwe,je hakuna wachezaji wengine kweli wazuri zaidi ya hawa tulio nao huko mikoani,achana na 'mapro' kwanza,nk

    3;Je kocha tuliye naye na mbinu zake ni sahihi?.Kocha hatafuti mechi za jaribio kama mwenzake aliyemtangulia,mechi za majaribio zimepungua;

    Bila mbinu za timu kushinda hatuwezi kuvuka.


    Mwisho,Timu ya michuzi nawashukuru sana kwa picha nzuri,wachezaji ninawapongeza kwa kuvuka hiki kigingi.Nyie wachezaji wetu,kama timu ya chad inawasumbua mtaweza kweli kupambana na hiyo miamba??

    David V

    ReplyDelete
  4. MPILA TUTACHEZA LINI, UBISHOO NA SIFA ZA KIJINGA NA MASIALA TUTAACHA LINI....????

    TUKO HURU MIAKA 50 SASA, II NDO TUNATAKA....

    mnafungwa na chad, alafu mnategemea kwenda world cup. Nyie vijana nendeni mkalime. Wachezaji mi na wambieni wako mikoani na sio apo mnapo hangaika kutafuta. Nakumbuka kipindi naishi dodoma miaka ya 96-97 tulikua na timu yetu ya mtaani inaitwa kizota, Yanga walikuja tukawaomba mechi uwanja wa magereza tukapiga nne, moja. simba wakaja tukapiga tatu bila. cda na waziri mkuu ndizo timu walikua wateja kwetu. Kocha alikua anaitwa john ndandala, jamaa alikua ni kocha anayefuatilia soca la mbele kama anaishi uolaya vile. na mazoezi yake yalikua makali sana. wachezaji aliowafundisha mpila ni kama msaga sumu, uyu simba uyu alikua kiboko ya simba wakija dodoma ada wakamchukua. Kulikua na kichwa inaitwa michael sudi ama zalau, jamaa design ya drogba ivi na alikua anacheza haijawai kutokea hakiya mungu apo bongo, sospeter, juma4, leo, luta uyu angekuja mrithi husen masha kwa uwezo wake wa kukamata mpila. shaka. daimon longopa beki isiyo pitikaga hata uloge. mode alikua anapigia kushoto alipigaga shuti likataka kumuuwa steven names, ulizieni, jamaa alikuwa anapasua nyavu mara kwa mara. dome nae mkomavu ka chuma. na wengine wengi tu sio lazima nitaje wote. kati ya hawa vijana waliishia kurogwa kama zalau, wengine walienda adi simba na yanga lakini nahisi uongozi na gundu la izo timu hatujaskia mambo matamu baada ya apo, na ingine ka wote hawa alikua kocha john ndandala ambaye aliishia kuwa padri nadhani. sababu ya kusema yote haya ni kuonyesha kuwa tanzania tunavyo chukulia vitu for granted. wenzetu sehemu nyingine kama uingereza ambako nimeishi sana watu wanahakikisha kila kipaji kinapatikana na kulitumikia taifa. hata uwe unakaa hastings, crawley, rye hata bexhil ama kijiji chochote kile watu watakuona cha msingi uwe na kipaji cha hali ya juu na sio lazima uishi london tu. Sisi tanzania nakuhakikishieni tukikatiza vijiji na vitongoji vyote vya hiyo nchi, tukiwa na ma talent scouts wa uhakika mtashangaa tuna pasua mbaya, unaweza kutana na jitu apo tz linaongea kinyaturu tu ata kiswahili halijui vizuri lakini ukilipa mpila utacheka ndugu yangu. Tuigeni mifano ya wenzetu, apo mimi nimetoa mfano tu ili kuleta uelewa wa ii mada. Nauhakika kuna watakao soma hii mada ambao wamewai kumuona ZALAU akicheza na kiukweli Tanzania stars haijawai kuwa na striker ambaye anaweza kufika kiwango hata nusu cha jamaaa. Ulizeni kwanini walimloga amekuwa chizi kabisaaaa sikuizi lakini bado siku akikatiza uwanjani nasikia kuna siku anaamua tu kucheza na bado analeta maajabu uwanjani. Mimi nahisi hata uchizi ulimjia baada ya kutoonekana na taifa, hakunaga mechi jamaa hajafunga goli. iwe tumecheza na simba au yanga.

    Kama tunataka ushindi wa kiukweli tz jamani ndugu zangu nawaomba chonde chonde tuende mikoani , vijijini, vitongojini kooooote tukaanze upya kutafuta akina ZALAU. Nauhakika bado wapo wa,mejaa tele. Awa vijana mabishoo tu. Hatutaki ubishoo tunataka ushindi. Hii unatuuma zaidi sie tulioko uku nje tunazalauliwa na wa nigeria na watu wengine kwanba taifa letu hatujui mpila hatuna vipaji vya mpila wakati sio ukweli. Hawa warudishwa ligi daraja la nne.Alafu tuanze kazi kama mwenge vile kijiji adi kijiji.

    Kaka MICHUZI na mabloger wenzio. NAOMBA MUI COPY II MADA NA UIWEKE KAMA HOJA YA HAJA NA TUONE WATANZANIA WENZANGU WANAFIKIRIA NINI.

    Kwakweli ii ishakuwa nishai sasa. Tunataka Maximo arudi sikatai lakini kwanza ii safu yetu waje watu waliotumwa kimpila na wenye machungu na nchi yao na sio kuleteana ubishoo tu apa mjini. Kwanza sala la taifa stars kuweka kambi kalibu na ambiace club, wapi na wapi. pale madudu yanajiuza daily, ngono njenje. Ivi sisi tunataka uushindi wa mpila au tumejenga bonge la uwanja ili watu wawe wanawanga mule.

    AU TUTABAKIGI KUBAHATISHA TU NA KISHA KUUMBUKA.
    Asanteni.

    MDAU......

    ReplyDelete
  5. vp kuhusu ubora au viwango vya wachezaji wetu?mpira wa sasa ni chini tu siyo mieleka,ndio maana hata David Silva au Neymer wanautandaza kweli kweli japokuwa ni vinjiti tu,sasa Ngasa sijui alikua anafanya nini hapa.
    Kama tunafungwa hata na Chad tu,tumtafute mganga mapeeeeeeeeeeeeeeeema.maana Ivery Coast na Moroco siyo timu za kuzibeza

    ReplyDelete
  6. Ligi ya Tanzania ngumu

    ReplyDelete
  7. kwa kweli mm sisemi lolote team yetu inatuvunja nguvu ss wabongo kila siku tunakuwa bado tupo nyuma na jamaa hapo aliposema ni bora yule kocha maximu harudi ni vizuri sana na kuna vijimambo furani jamani tuwekani wazi umnajuwa hawa makocha wanakuwa wanaingiliwa kazi zao na watu walio karibu na hii team yetu ya taifa na kuwachanganya walimu hao ila tusimlahumu huyu babu mjuwe kuna vigogo vipo hapo hanataka huyu acheze huyu ascheze yaani nnoma jamani tujitahidi nasi tujigambe ugenini mmeshinda nyumbabi tena tunafungwa si aibu hii aaaah!

    MDAU UGIRIKI

    ReplyDelete
  8. Kweli kabisa mdau wa juu, this time Michuzi ameleta quality pictures.

    ReplyDelete
  9. Uyo mdau aliye andika sana apo juu anaonekana kuwa na machungu sana na ii timu. Ni kweli kabisa tanzania kuna vipaji vingi tu. Ningependa kuongeza kuwa na makocha tunaowaleta pia tusiwaingilie kazi zao. Tuwaache wafanye uamuzi wenyewe. Watu wengine walio karibu sana na timu yetu wafukuzwe tumuachie kazi kocha. Na kama kuna kipaji sehemu yoyote nchini basi kocha ataarifiwe ili aweze kukicheki kama kina kiwango kinacho itajika. Maana tunaweza ona ngasa ndo mwenyewe kumbe wenyewe wa ukweli wanaishia kuwa machinga tu.

    ReplyDelete
  10. Hapo Ngasa alikuwa anakupa..."Yan kibadach...yan shotokan...kapau..."

    ReplyDelete
  11. Hakuna liwalo tunaendelea kuona, kama kawaida tu hakuna mpya. Mbinu ni ile ile tu ya kuwaanda vijana mapema kuanzia mashuleni na hadi level zingine za juu, bila kusahau professional soccer schools ili tuengeze uwezo wa vipaji na mbinu zilizobobea kitaalamu na uzowefu wa kusakata kabumbu.

    Kwa matayarisho ya zima moto timu haifiki popote na mamilioni ya shilling kupotea tu. Narejea tena NGOJA TUONE,hata hivyo siachi kuwapa hongera kwa kufuzu hatua moja kiaina.

    ReplyDelete
  12. Kwenye kutafuta tiketi ya fainali za CAF babu katuburutisha mkia tofauti na Maximo aliyekuwa anatushikisha nafasi ya tatu.
    Timu inayohangaika kama Chad nayo inakuja na kutupa kichapo kwenye wanja letu jipya la Taifa. Enzi za Maximo waliokuwa wanaweza kutufunga Taifa ni timu zilizotuzidi kisoka kwa mujibu wa FIFA.
    Mwenye macho haambiwi tazama. Babu atupiwe virago. Maximo arudi kuendeleza alipoishia. Kadri babu anavyozidi kukaa na timu ndivyo inavyozidi kuboronga.

    ReplyDelete
  13. WACHEZAJI MABISHOO,HATA AJE KOCHA GANI TUTAFUNGWA; MCHEZAJI ANAUKIMBILIA MPIRA KIDOLE JUU; OVYO KABISA KAMA MPIRA ATA SISI TUMECHEZA; WA KUWABADILISHA NI WACHEZAJI SIYO KOCHA:

    ReplyDelete
  14. Aisee mdau uliyeandika saana hapo juuu, uko sahihi kabisa, mi nimekulia Majengo Dodoma, ukivuka tu reli unafika kwa kina abdallah mwaipaya....Yaani huyo JAMAA anaeitwa ZARAU, alikuwa noma ile mbaya, aliujua mpira balaaaa, nna uhakika hakuna mtu amewahi kutokea kuujua mpira kama yule jamaa bongo nzima, ZARAU alikuwa noooooooooma. Kina Stanley sungura sijui wako wape wale, alikuwa mzuri sana wingi ya kushoto lakini kwa ZARAU wote walikaa wale. Nataman sana nimuone ZARAU. Yaan nadiriki hata kumfananisha ZARAU na mchezaji mwingine yeyote Africa hii, yaani labda Kanu enzi ziiile 1996-1999,
    aisee umenkumbusha zaaman sana mkuu hapo juu.

    ReplyDelete
  15. Wakati Maximo yuko Bongo, mimi nilikuwa naamini Stars watashinda. Walipokuwa wanashindwa nguvu walitoka droo. Hata mabao waliyokuwa wanafungwa hayakuzidi zaidi ya bao moja. Halafu fainali zijazo zafanyika Brazil. Maximo arudishwe jamani!

    ReplyDelete
  16. Wa TZ inapaswa tuelewe kwamba

    1. Uwezo wetu wa football ni mdogo sana.

    2. Hatukuwahi kuwa na kiwango cha juu, challenge tulichukua 74 akaja Mzirai kachukua 94 (after 20 years). Kenya na Uganda wamechukua mara kibao.

    3. Hata Simba ba Yanga hakuna kitu kabisa, ni afadhali timu ya taifa. Gormahia wamechukua kombe la washindi Afrika na Villa wafika fainali ligi ya mabingwa. Simba kufika hiyo fainali tena ya kombe dogo (CAF) imekuwa nongwa.

    4. Hata akija Mourinho bado hatafanya lolote.

    5. Hatuna lolote ni mameno tu.

    6. Na sio football tu, hakuna mchezo tunaweza sema tunaujua. Hata mchezo wa kutemeba ama kulenga shabaha au kurusha mkuki huwa tunakuwa wa mwisho kila siku.

    CHAKUFANYA

    Tubadilike, tuwe na mipango endelevu, shule za michezo, uwekezaji kwenye michezo, tuache uswahili mpirani, tuendeshe mambo yetu kisasa. Tuwe na vision na mission vinavyotekelezeka.

    Vinginevyo

    Tutaendelea hivi miaka yote wakati wenzetu wamekwisha piga hatua.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...