Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi mteule wa Ufaransa nchini Tanzania Mh Marcel Escure leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi mteule wa Ufaransa Mh Marcel Escure baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam
Baada ya Kupokea hati ya utambulisho, Rais Dkt Jakaya Kikwete akimtambulisha balozi mteule wa Uswisi nchini Tanzania Mh Oliver Chave kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha ambaye anafuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Bi. Grace Shangali na Mkurugenzi Msaidizi katika idara hiyo.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na balozi mteule wa Uswisi nchini Tanzania Mh Oliver Chave baada ya kupokea hati ya utambulisho.Picha na Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. jamani hii inakuwa hawi heshima rais kumuita just rais jakaya kikwete? drt ikiachwa kuwekwa hatakuwa rais au mpaka watu wajuwe nyeye ni dr,acheni kulimbikizia majina watu bwana.jina la rais j,kikwete linatosha sana.hahahaha mheshimiwa dr jakaya mrisho kikwete.

    ReplyDelete
  2. anaitwa Grace Shangali rekebisha

    ReplyDelete
  3. Hawa wafaransa ndio wale waliokumbatia waasi wa libya hadi kmuuuwa cl Muammal Gadhaffi. Vipi SMT inaikataa serikali mpya ya Libya na kuwakaribisha Ufaransa nchini. Hahahaa! kweli hawa wakubwa wanaoogopwa.

    ReplyDelete
  4. Anonymous Wed Nov 16, 04:03:00 AM 2011 kwani ugomvi? tafadhali jifunze kutumia maneno kama tafadhali, naomba, nk

    ReplyDelete
  5. duh hawa wafaransa mimi nawaogopa sana,manake ni wataalam wa kugombanisha vi nchi vya Africa,Rwnd & Burnd n.k anyway karibu sana mheshimiwa barozi kwa wadanganyika,bara la africa ni lenu mnaweza kwenda popote na kufanya vyovyote mpendavyo hatuna cha kuwafanya ila mungu atayanyoosha mapito yake na hakika mtauona mkono wa chuma.

    ReplyDelete
  6. Wafaransa hawa kuweza kugombanisha wanawamudu hao hao Banyamulenge huko Rwanda ,Burundi...Tumeshawastukia Hapa kwetu NO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...