Baadhi ya Wahitimu wa MUM waliopokea Nondozz zao jana katika Chuo Kikuu cha Kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu hicho cha Kiislamu kilichopo mjini Morogoro. Mkuu wa Chuo hicho, Mama Mwatumu Malale alitunuku shahada ya kwanza kwa wahitimu 272 wa fani mbalimbali za kielimu.
Baadhi ya Wahitimu wa MUM wakisubiria kupata Nondozz zao jana katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha mjini Morogoro.Picha na Mdau wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongereeni sana wote.Binafsi nilikuwa sikifahamu vizuri hiki..Imebidi niingie kwenye google haraka sana.Kuna kozi nzuri nzuri nileona kwenye website ya chuo.Mna bahati sana nyie mnaosoma enzi hizi..zamani kupata elimu ya chuo kikuu ilikuwa kazi sana.kufaulu la darasa la saba huko vijijini ilikuwa mwanafunzi mmoja au wawili tarafa nzima.Ilikuwa 'issue'

    David V

    ReplyDelete
  2. Wadada wa kiislam wamependeza...final waislam tunajikombowa na dhulma iliyosimikwa na Nyerere...ktk upande wa elimu..eti tunaambiwaga waislam hawajasoma ndio maana wengi hawako serikalini...baraza la mitihani linashikiliwa na asilimia kubwa na upande wa kushoto..wewe upande wa kulia utapitishwa kweli? najuwa mtasema naongelea udini itakuwa jiwe gizani..ukilia tuu limekupata nawe ndiye utakuwa mdini..

    ReplyDelete
  3. mtamaliza maneno wenzenu wanazidi kuongeza vyuo

    ReplyDelete
  4. Chuo kinafundisha kozi gani na vigezo gani vya kuingia maana naona mavazi ya akina dada kama ya dini fulani!!

    ReplyDelete
  5. Yap kama yalivyo mavazi ya kisista! Ukitaka kuwa sista si lazima uvae kama sista wa kikatoliki au utaenda kusoma na majeans yako? Watu wengine bwana?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...