Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohamed Ali, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohamed Ali, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi mpya wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzona kujitambulisha leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo na kujitambulisha leo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Yaani huwa nikimwona Dr.Bilal huwa nakumbuka kitu kimoja tu.Mwaka 1994(Sept-Oct) wale mliokuwa UDSM mlimani mnakumbuka wakati tumeandamana kutoka chuoni kwenda wizara ya Sayansi sijui na teknolojia,Doc akiwa Katibu mkuu alitoka nje ya ofisi kuja kutuhutubia,wakati akiendelea kutuhutubia akiwa kasimama juu ya "stuli"kuna mtaalam fulani akaenda akaipiga ngwara ile stuli..kilichotokea hapo siwezi kukisimulia hapa.Ilikuwa balaa sijawahi kuona.

    David V

    ReplyDelete
  2. Sudan ipi mboni hamuweki wazi? maana sote tunajua kuna Sudan kaskazini na Kusini muwe makini tafadhali!

    ReplyDelete
  3. Kuna nchi za Sudan na Sudan ya kusini

    ReplyDelete
  4. Ofisi ya Mheshimiwa balozi Masaki Okada iko Upanga kama sikosei. Nataraji makazi ya Mheshimiwa Masaki yatakuwa Masaki kama yalivyo makazi ya mabalozi wengi jijini Dar na bila shaka atakuwa anjisikia yuko nyumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...