Habari tulizozipata punde zinasema kuwa,mshindi wa tuzo wa Nobel na rais wa zamani wa Finland,Rais Martti Ahtisaari (pichani) ndiye atakaekuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania zitakazofanyika tarehe 9.12.2011 katika Jiji la Helsinki Finland. Ni heshima kubwa kwake kualikwa katika sherehe hizi kwani Tanzania ni nchi aliyopata kuishi akiwa kama balozi wa nchi yake miaka ya nyuma, ni sehemu muhimu katika historia yake binafsi na maisha yake ya kikazi
Home
Unlabelled
Martti Ahtisaari Mgeni Rasmi Sherehe za Uhuru wa Tanzania Helsinki-Finland
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ni sherehe za miaka 50 ya huru wa Tanzania au uhuru wa Tanganyika? Sikumbuki Tanzania kupata uhuru,ninavyofahamu ni kwamba Tanganyika ndio iliyopata Uhuru.
ReplyDeletemdau wa kwanza, nakubaliana na wewe! ni kweli tanzania haijawahi pata uhuru kwani ni united country.
ReplyDeleteAcheni upuuzi , Tanganyika , Tanzania same same tofauti hipo wapi ,wewe unazani ukisema Tanganyika wangapi wanaijua Tanganyika , kambo ya kupoteza muda kuwaeleza history akuna.Acheni ubaguzi na ninauakika mnao guna guna ni wa zenchi , kwani wabara hatuna time Tanganyika iwe Tanzania mule hule tu ,sisi tunaangalia mbele.
ReplyDeleteMdau Paris
Hata hivyo si dhani kwamba uhuru huo tunao tena, kwani Tanganyika si imeshagawanywa vipande vipande na kutawaliwa tena na wakoloni kwa kile kinachoitwa WAWEKEZAJI. Mfano Loliondo n.k.
ReplyDeleteTUNAMDANGANYA MARTTI AHTISARI KWAMBA TUNA UHURU WA MIAKA 50.
Nikupongeze mdau wa kwanza hapo juu kwa kuwakumbusha hili. mimi binafsi nashangaa sana ninapoonaa hili jambo likipotoshwa tena hata na vyombo vya habari tunavyoviheshimu kuwa ni makini vimekuwa vikirudia hilo kosa kila leo. wanasahau kuwa kila ifikapo mwezi wa nne huwa tunasheherekea kuundwa kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuwa 9 december na 26 April ni vitu viwili tofauti. vizuri tutaendelea kuwakumbusha mpaka wataelewa tu kabla ya hiyo 9 December
ReplyDeleteNaomba contacts za wandaaji wa hii shughuli. Asante.
ReplyDeleteSamweli
Wadau wa Helsinki kwa nini msingemualika yule jamaa Teuvo Hakkarainen naye ni mpiganaji mzuri tuu.
ReplyDeleteTanganyika ndio ilipata UHURU tarehe 9 dec 1961, Sio tanzania ! Aisee naona wewe umezaliwa mwaka 1981 miaka 20 baada ya uhuru wa Tanganyika
ReplyDeleteTutake tusitake ndoa ipo palepele,,,Zanzibar wana ile kitu sitaki nataka, wanalalamika hawataki Muungano huku maslahi ya Muungano kama kugawana vitu 50% kwa 50% bila kuzingatia kuwa wao kwao ni sehemu ndogo ki Jiografia na hata pia ktk Uwakilishi!!!
ReplyDeleteHawa watu wa visiwani
wananufaika sana na Muungano, mfano misaada inayokuwa kwao kwa jina la Zanzibar sisi hatutii maguu kabisaaaa, ila misaada inayokuja kwa Jamhuri ya Muungano wanataka nusu kwa nusu bila kujali wao ni sehemu ndogo sana ya Tanzania!..Ila ndio kama hivyo wamebaki na sitaki nataka yao kwa vile wanajua wazi kuwa wananufaika sana tu!
Wewe anonymous wa Tue Nov 15, 02:44:00 PM 2011
ReplyDeleteUnajidai Bara (Tanganyika) na Zanzibar zinagawana sawa kwa sawa na kua Zanzibar ndio inayofaidika na Muungano, swali kwa nini watetezi wa Muungano watoke Tanganyika tu? Unakumbuka kuwa Muungano feki ulianzishwa kwa mambo 11 tu baada ya Nyerere kumstisha Karume kama atapinduliwa (atampindua). Unajua kama shauri la Muungano lililetwa na Nyerer kiujanja? Unajua Karume alitaka kuvunja Muungano ndipo akauliwa? Je unajua kama mambo ya Muungano kwa sasa ni 22? Je unajua kama hio nyongeza yote imependekezwa na watu wa Bara? Ikiwa unaona Zanzibar ndio inayofaidika, basi tafadhali vunjeni ili sisi tusifaidike tena muendelee na huo utajiri wenu. Nakushangaeni nchi inayoshindw ahata kusomesha watoto wake kiwnago cha msingi inakuwa na majivuno kiasi hicho. Vunjeni Muungano kama mnaweza, sisi hatuutaki hata kuusikia.
Wasia wangu kwa wale ambao hawaoni haja ya kuisika Tanganyika yao. Wasawhili wanasema mkataa kwao Mtumwa, kateni nchi yenu, sisi yetu tunayo na tunaendlea na mapambano hado uhuru wetu tutakpouchukua tena. Wakati huo mtakuja kujua kama nyinyi ni Tanzania au Tanganyika.
Hongera nyingi kwa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Finland. Bila shaka ni heshima mliyonayo kwa wenyeji wenu ndio inayowafanya muweze kuungana na Rais Artisaari katika shughuli hii. Serikali kupitia wizara itajitahidi kuwa pamoja nanyi katika jitihada kama hizi mnazozionyesha. Nawatakia maandalizi mema. Benard Membe (MB).
ReplyDeleteWaandaji ni Jumuiya ya Watanzania, mimi ni mwanachama, nimekuwa nikifuatilia maandalizi ya hii shughuli kupitia facebook, wewe kama ni member jaribu kuingia (suomi tansania seura) kama sijakosea spelling.
ReplyDeleteKwa mujibu wa redio clouds jioni hii wamesema Hakkarainen naye atakuwa ndani ya nyumba. JJ
ReplyDeleteMdau wa hapo naona chuki binafsi, mwongo ni wewe ambaye unabeba ganda la kijani, unadai siku zote haki zako kutoka serikani, kama Uhuru hatunao kwa nini usiombe hizokutoka kwa wawekezaji?
ReplyDeleteNa sisi pia huku Oulu na jamaa zetu wa Lapenranta tungependa kuja kujumuika nanyi huko Helsinki. Waandaaji tujulisheni utaratibu.
ReplyDeleteAnonymous: Unajidai Bara(Tanganyika) na Zanzibar zinagawana sawa.........
ReplyDeleteNyinyi Wa Zanzibar ni wakorofi sana na hamna shukrani, wabaguzi na hamfikirii, mmelalamika Serikali ya Kitaifa mmeipata sasa Maalim Seif anavaa suti za serikali na ni kiongozi wa Serikali bado mnachonga...suala ni kuwa Zanzibar ninyi ni wavivu sana hamtaki kazi ngumu,,,,Maalim Seif alikuwa na malalamiko kabla tokea apate MADARAKA MBONA HADAI KUWA ZANZIBAR IJITENGE???...kimya!!!,,,,kwisha MUUNGANO HAUFI KWA VILE VIONGOZI WENU WANAUPENDA NA WANAJUA SIRI NZITO YA FAIDA ZINAZOPATIKANA.
Hongereni sana kwa maandalizi ya shughuli hiyo. Nawatakia kila la kheri na nawashukuru sana watanzania muishio Helsinki Finland kwa ukarimu mlionionyesha nilipokuwa nikisoma huko mwaka huu.Naamini sherehe hii itafanyikia pale pale PASILA.
ReplyDeleteVioleth, UDSM - Tanzania