Marehemu Mama Mwingira enzi za uhai wake
Imetimia Mwaka mmoja tangu utuage Mama.  Ni simanzi isiyoelezeka! Kila kukicha tunaona kama ndoto Mama. 

Ni vugumu kukubali hili pamoja kwamba ni mwaka sasa…Tunakupenda   mama, tunakukumbuka sana, Mama yako Sabina  anakukumbuka sana, tunamlea kwa Upendo wote  mama.
Mama   ulijitoa kwa kila hali hadi kufa kwa ajili yetu Watoto wako (Upendo, Edmund, Josephine,Sabina, Cassian, Wilfred and Cecilia).Tunakumbuka mafunzo yako  ya “Upendo  usio na masharti “na mshikamano. Tunakuombea  Mama nawe uzidi kutuombea. Tutakuenzi Daima Milele ….
Asante sana sana Mama!!
Wajukuu  wako (Gladys, GloriousMary, Edmond, Andreas, Crystaline, Cassian, Olivia na Prince John) wanauliza  “bibi mbona hurudi ??”
Unakumbukwa pia na shemeji, wifi, wadogo zako, marafiki, ndugu,Majirani na Jamaa wote Mama. Sote tunabubujikwa na machozi mazito Mama.
Familia ya Marehemu John na Mary Mwingira wa Upanga ,Familia ya Dr Edmund Ndalama wa Kunduchi ,Dar salaam, pamoja na ndugu na jamaa wote wanapenda  kuwaalika wote kwenye Misa Takatifu itakayofanyika Tarehe 19 Novemba 2011,Saa 5 kamili asubuhi, Kunduchi SEAMIC  road plot 390/1, (Nyumbani kwa Dr Ndalama.)
Karibuni  wote tumuombee  Mpendwa wetu Mary John Mwingira.
 MUNGU AKUPAZE PEMA PEOPONI   MAMA MPENDWA MARY  JOHN MWINGIRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. RIP mama! Ulikuwa mtetezi wa wanyonge

    ReplyDelete
  2. RIP mama Mwingira

    ReplyDelete
  3. mungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi, daima tunakukumbuka mkwe wetu tunaona kama umesafiri na siku moja utakuja tutembelea kama ilivyokuwa kawaida yako.

    ReplyDelete
  4. Pole sana watoto wa Mama Mwingira. RIP mama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...