Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo ambapo alisomewa jumla ya mashitaka matatu likiwemo la kushindwa kutoa taarifa sahihi za matumizi ya vitu mbalimbali vya shirika hilo.Bw. Mataka ameachiwa kwa Dhamana ya Sh. Mil. 20 kutoka kwa wadhamini wawili tofauti ambao kila mmoja amemdhamini kwa sh. Mil. 10.
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka akisindikizwa na askari Polisi wakati akitoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo alikosomewa mashtaka matatu likiwemo la kushindwa kutoa taarifa sahihi za matumizi ya vitu mbalimbali vya shirika hilo.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.
Hana hatia mwachieni! Si kawaida yenu?
ReplyDeleteWa UDA naye lini atafikishwa kizimbani?
ReplyDeleteangetiwa ndani filauni huyu, masela wamuonje
ReplyDeleteSerikali msimhukumu mataka kwa kushindwa kuweka kumbukumbu za matumizi ya vitu. Jihukumuni ninyi wenyewe ambao mmeshindwa kuliendesha shirika hilo kibiashara hata kabla ya Mataka.
ReplyDeletePole sana Davi, ungekuwa unakula na kuchangia chama usingefikishwa hapo ulipo.
ReplyDeleteHuyu hausuiki moja moja na kuporomoka kwa shirika letu la ndege...
ReplyDeletekwa suala la kupeleka wakubwa mahakamani JK anajitaidi tumpongeze kwa hili
ReplyDeleteHali imebadilika siku hizi. Kigogo unaburuzwa mahakamani! Enzi za nanihii, unabadilishiwa post tu!
ReplyDeleteKuburuzwa mahakamani ni one thing, nia ya dhati (kwa serikali) na hukumu ya HAKI (kwa mahakama) ni another!
ReplyDeleteda! how much money involved? vijisenti au?
ReplyDeletekatiba iweke kifungu cha kutokuwepo kinga yakushtakiwa Rais na viongozi wa juu ili nao waonje machungu ya utamu wao wakiwa madarakani
ReplyDeleteDuh kama siamini amini vile....mbona jamaa kajenga majengo ya ppf mawili, au na kule kachakaua nini mmmh....audit ipite tena ile ya PWC pale PPF....hueonda wakaibua mengi juu yake..
ReplyDeletePengine alikuwa anakula peke yake!!
ReplyDeleteMie nafurahi kitu kimoja kwamba generation iliyopo na labda inayokuja hawapendi mafisadi. Wakiingia madarakani basi mafisadi wanalo..si mnaona kule misri..ni young generation!
ReplyDeleteAnon wa 04:43:00, ndiyo, kuburuzwa mahakamani ni one thing. Nayo ni hatua nzuri tu, Tena ni kubwa sana ukilinganisha na mtu akichafua sehemu anapelekwa kwingine na kuendelea kuchafua. Binafsi naiponeza sana serikali hii kwa angalau kuanza na hatua hii ya kwanza. Labda akina Mbowe wakiingia wataendeleza hatua ya pili na ya tatu (we hope!)
ReplyDeleteAlikula peke yake sana. Hebu angalieni maisha anayoishi na magari aliyekua nayo. Ile nyumba yake ya mbezi beach mnaijua wadau? Kama si mwizi hujengi kitu kama kile. Swali ni je? Haki itatendeka? Hakimu au mahakimu wana aminika?
ReplyDeleteHaki haitatendeka. Mahakama zetu tunazijua!
ReplyDeleteHuyu nae wanamuonea tu. Wanamtoa kama sadaka ili kujisafi.
ReplyDeleteHE WHO HAS NO SIN, LET HIM CAST THE FIRST STONE!
David, God will help you in this mess. We know they are dirty than you.
Wengi watakuwa wameumia ktk ATCL, hiyo PPF na kwingineko alikopita.... kwa udhamini wake wa kampuni ya mtandao, kwa kupenda watu wamwelekee kinyume nyume!
ReplyDeleteBosi amekuwa na tambiko ya ajabu sana!
Wengi watakuwa wameumia ktk ATCL, hiyo PPF na kwingineko alikopita.... kwa udhamini wake wa kampuni ya mtandao, kwa kupenda watu wamwelekee kinyume nyume!
ReplyDeleteBosi amekuwa na tambiko ya ajabu sana!
Safi sana, tena akatokomee huko jela na kundi lake, halafu mbona kosa limetajwa moja?Habari ya mahujaji je?Ndege ya Airbus iliyofilisi kampuni?ajira kimya kimya karibu watu mia, bila ya kutangaza.uozo ni mwingi
ReplyDeleteHakuna uhakika kwamba eti kwa kuwa wewe ni kijana, basi hupendi ufisadi! kuna vijana/watu wengi ambao wanaonekana kutopenda ufisadi lakini mara tu wao wanapopewa nafasi hujikuta nao wakiendeleza ufisadi kwa kwenda mbele!
ReplyDeleteUfisadi na fujo ni ugonjwa wa kudumu wa mtu mweusi kama anony mmoja hapo juu alivyosema. Leo huna wadhifa unajidai mwaminifu na kuwazomea wengine. Siku wewe ukipewa nafasi huwi fisadi ila nyang'au. Nyang'au ni mbovu zaidi ya fisadi maana nyang'au habakishi.
ReplyDeleteHaya na tutoke nje ya mipaka yetu kidogo. Angalia mambo anayoyafanya jamaa mpya pale kwa Farao sasa hivi. Hata mwaka haujapita, anarudia makosa yale yale, yanayoweza kumfanya kesho ajute kuzaliwa. Hawa watu wanapokuwa kwenye viti wanakuwa wapumbavu au wanadhani wao ndiyo walioumba mbingu na nchi!
Mara kwa mara nikimkumbuka Baba wa Taifa na kumfikilia saana, huwa simmalizi. Mzee yule alikuwa shuma mtupu walahi!RIP.