Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini 
John Tendwa
Na Magreth Kinabo – Maelezo

MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini John Tendwa , amevitaka baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa , wanachama na washabiki wa vyama husika kuzingatia sheria za nchi na sheria nyinginezo.

Aidha msajili huyo, amesema kuwa ni wakati mzuri wa kutenganisha mipaka ya vyama na mamlaka ya serikali kwa kutambua kwamba ipo mihimili mitatu ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama ambayo kila mmoja umepewa ukomo wake kimamlaka.

Kauli hiyo imetolewa leo na Tendwa kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, kufuatilia vurugu zilizojitokeza nchini ambazo zinasababishwa na baadhi ya watu hao.

“Vurugu hizi hazina tija kwa taifa na zinasababisha uvunjifu wa amani na kupelekea wananchi kutoshiriki katika shughuli za uzalishaji kwa kuwa muda wote wako kwenye mikusanyiko na wengine kuhofiwa kuathiriwa na matokeo ya vurugu hizo.

Aliongeza kuwa viongozi wa vyama vya siasa kuingilia uongozi na usimamizi wa mihimili hiyo ni kinyume na kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi, kitendo ambacho mamlaka husika lazima zikidhibiti.

Hivyo inapotokea mamlaka zikichukua hatua si busara kuanza kulalamika kwani kila mamlaka inao wajibu katika jamii.

“ Hivyo basi Msajili wa Vyama Vya Siasa hayuko tayari kuvumilia hali hii ya uvunjifu wa sheria ya usajili wa vyama vya siasa ambayo vyama vyote vina wajibu wa kuzingatia katika utekelezaji wa kila siku wa shughuli za vyama vyao,” alisisitiza.

Alisema endapo chama chochote kinaona hakikutendewa haki katika jambo lolote na muhimili wowote kama Bunge, Serikali au Mahakama ni vyema kufuata sheria, taratibu za kisheria kuwasilisha malalamiko yao sehemu husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wapi bwaana hizi ni kelele za chura tembo anaendelea kunywa maji! CCM ni mchochezi mkubwa wa vurugu wakitumia njia za mabavu kuwakandamiza wenzao wa CHADEMA hapo ndo kwenye tatizo kubwa. Serikali imenyamaza kimya ikisubiri polisi ndo watatue matatizo ya kisiasa! Polisi lazima watumie nguvu kuleta amani na wala sio wa kulaumiwa kwani wanazidiwa nguvu na wananchi inabidi wajitetee. Matatizo haya yanawezekana kumalizika kidiplomasia sio kwa kutumia mabavu na mbinu za kukandamizana zilizopitwa na wakati. Ankal kama utaona kwamba nimesema sana kweli unaweza ukaiprint hii na kuwapelekea wahusika inaweza ikasaidia kuliko kuiweka kapuni please acha ujumbe huu ufike kunakohusika.

    ReplyDelete
  2. Michuzi, Huyu Tendwa anasukumwa na Ukada. Awambie CCM, wawe tayari kutengeneza katiba itakayoleta manufaa kwa watu wote waache ufisadi, rushwa waache kuiba kura siyo kuegemea upande mmoja CCM ndiyo haitakii mema nci yetu, inafanya ukandamizaji. Mbona walipoiba kura haukusema sasa unasema nini.

    ReplyDelete
  3. CCM wanatumia mabavu na ukandamizaji ili kuwanyamazisha wa vyama vya upinzani. Hata watoto wadogo wanayaona sembuse watu wenye akili zao! Sasa watu kama msajili wa vyama vya siasa wana wajibu mkubwa wa kusema bila kupendelea upande wowote lakini nionavyo mimi anaongea kwa kukipendelea CCM. Siasa za kukandamizana zimepitwa na wakati, watu wame elimika na wameamka wanazitambua haki zao na wanjua kutafsiri sheria.
    Malalamiko yote yanayotolewa na wapinzani ni ya ukweli kabisa na hakuna mtu anaye pinga. Mifano michache tu ni Maisha kuwa magumu kwa watanzania, rushwa isiyo koma, wizi wa fedha za EPA,Richmond na Dowans,Mikataba mibovu, Kutorosha wanyama pori, njia za ujanja ujanja za kutaka kutunga katiba itakayo iweka CCM madarakani milele,Upendeleo wa wazi wa spika wa bunge bungeni, Kuwakandamiza watanzania wazawa na kuwakumbatia wawekezaji,Matumizi kandamizi ya vyombo vya dola kama polisi na usalama wa taifa, kuingilia uhuru wa mahakama, ufujaji wa fedha za wananchi katika halmashauri, uuzaji wa UDA na mengine mengi tu yanamfanya mtu ajiulize serikali imekwenda wapi? Hawayaoni!? Hawayasikii!? kama wanayasikia na kuyaona mbona wamekaa kimya?? Je,wako kimya kwasababu nao ni wahusika katika madhambi haya? Vyama vya upinzani vipo kwa ajili ya kukikosoa cham kilicho madarakani na kwa jinsi tunavyo ona sasa hivi ni kwamba wapinzani wakikosoa wanabezwa au wanaitwa wana uchu wa madaraka, wanaleta vurugu nk. Bungeni ambako tungetarajia mambo haya yachukuliwe kwa uzito unao stahili nako ni mzaha tu, wabunge wa CCM wanaswagwa na kuwekwa kundi moja ili wapaze sauti ya Ndiyoooo au Hapanaa! Inashangaza hakuna kabisa mwenye mawazo tofauti na ya wakuu wao katika chama?! Kwa hali hii na jinsi tunavyo ona serikali haiko makini, kila mtu akijisemea lake na kutoa matamko kila kukicha- ni dalili mbaya. Mafuta ya petroli yanazidi kumwagiwa kwenye kuni na tuendako itachukua cheche moja tu ili moto ulipuke. Kuna mifano ya mataifa yaliyokuwa na nguvu na ukandamizaji kwa kutumia polisi, jela na mauaji lakini walishindwa na wananchi. Mimi binafsi nisingependa tufike huko. Kwa kuamini kuwa propaganda itawasaidia zaidi CCM wamekuwa wakipindisha ukweli na kukisingizia CHADEMA kwa kila kitu kibaya ili waonekane wabaya mbele ya macho ya wananchi. lakini wananchi wanafahamu ni nani asiye wajibika na ni nani aliye upande wa mafisadi. Lolote likija kuharibika CCM mtabeba lawama! Nyinyi ni wazoefu katika siasa tulitarajia nyinyi ndiyo muwe msitari wa mbele kujaribu kumaliza malumbano kwa hoja na diplomasia lakini mnacho kifanya sasa ni kinyume na inawashushia heshima wote! Msizishinikize taasisi za walipa kodi au vyombo vya dola kuwatetea, tumieni uzoefu wenu kisiasa kutatua matatizo pia malizeni kero za wananchi ili wapinzani wasiwe na cha kusema, zaidi ya hapo CHADEMA wataungwa mkono daima.
    Mau Tinga

    ReplyDelete
  4. sasa ndugu yangu hapo juu ulitaka ccm wafanyenini kuongea na watu wa ajabu ajabu?maana cadema inaongozwa na watu wa ajabu ajabu nikisema watu wa namna hiyo utakuwa umenielewa kumbuka kwanza sio vijana wote tunaipenda chadema no wala sio chama kinachoungwa mkono na watanzania wote wenyeshida na dhiki tupo wengi lkn njaa zetu tunazitafutia ufumbuzi wenyewe hatutegemei serikali ccm wala chadema nduguyangu kila mtu atazikwa kwenye kaburi lake siku itakapo fika hatutazikwa wote dhiki na shida yangu haiwezi tatuliwa na chadema ccm wala serikali

    ReplyDelete
  5. Hana kitu huyo Tendwa.Tulishamzoea

    David V

    ReplyDelete
  6. tendwa hapa ishu sio chadema laa!!!hapa swala ni kupambana kupata katiba mpya ambayo kila mtanzania bila kijali hali,kipato,rangi,umri nk wanashiriki si kama ccm walivyotufanyia juzi bungeni sasa inabidi tuandamane kusudi tuuambie umma ukweli halisi shilingi yazidi shuka dhamani dola sasa 1800/kila bidhaa sasa zinauzwa kwa dola bado sembe tu nalo halina mda mrefu its at the door tendwa wayajua haya?

    ReplyDelete
  7. Nimekuelewa ndugu yangu hapo juu. Tena hayo ya kuwaita wa upande mwingine 'Wa ajabu ajabu' ndicho kinacho tupoteza. Huko ndiko kunaitwa kubeza kama nilivyokwisha kusema. Hata kama kichaa anabwabwaja ukitulia na kumsikiliza utakuta kuna mambo mengine ya maana anayosema. Kusema tu 'huyo ni kichaa mwacheni msimsikilize' haisaidii. Hata shetani kule ahera ana uzuri wake.
    CHADEMA siyo miungu nakubaliana na wewe. Wanayo makosa na mapungufu yao lakini kwa kiasi kikubwa wanasema mambo ya kweli. Nani katika Tanzania atakataa kuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anatumikishwa pasipo na manufaa? Anaambiwa aka kague na akisha gundua upotevu mkubwa wa pesa anatoa taarifa halafu inawekwa kapuni. Pesa hizi hazija yeyuka bali kunakuwa na watu walio ziiba. Tunachotaka kuona watanzania ni serikali iliyo na meno, watu waogope kuiba. Leo hii watu wakigundulika wameiba wanahamishwa.
    Ndugu yangu najua hutaki kulalamika, lakini je hivyo ndivyo tutakavyo jenga nchi? sitaki serikali initunzie wanagu lakini ningependa serikali iniwekee mazingira mazuri ili niweze kufikiri na kufanya mambo yangu bila vikwazo wala kuogopa. Pesa zinazo ibwa ndiyo zinaweza kutumika kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo yetu sisi wananchi. Nafahamu sana kuwa wananchi wote si wana CHADEMA kwani ndivyo demokrasia ilivyo, lakini pia kuwa upande fulani kiitikadi isije ikawa inatufanya tutetee kila lililo baya likifanywa na chama unacho shabikia. Tukumbuke kuwa vyama vitaondoka siku moja lakini Tanzania itabaki. Pia nashindwa kukuelewa kwani wewe unajiweka pembeni kwa kusema uoza wanao upinga CHADEMA na wazalendo wengine wewe hayakuhusu!! Endelea na mawazo kama hayo hadi utakapokuja kuona huna haki yoyote ile katika nchi yako mwenyewe. Namalizia kwa kusema mimi sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini mimi ni Mtanzania kwanza na ninataka kubaki hivi.
    Mau Tinga

    ReplyDelete
  8. Je huy msajili wa mahakama anaishiwapi?I mekuwaje akapewa madaraka makubwa kama hayo wakati hajui hali halisi ya nchianayoishi?Hujui kuwa mahakama zetu na vyombo vya sheria vimejaa rushwa,uonevu na wanatetea chama tawala.Hivi ndio vinasababisha vurugu,vyombo vya dola vingekua vinatenda haki kwa wananchi wake wote watu wasingefanya vurugu,hii ni njia ya kuwashitua kwamba zile enzi za kuoneana ambazo zilizuka kuanzia awamu ya kwanza iishe watu hawazikubali.

    ReplyDelete
  9. Msajili ana boa ajabu, kwenye mambo ya maana hasemia subiri siku CDM wafanye jambo mbio utamsikia akisema, tumemchoka hana jipya kama mnakumbuka pale Igunga kama ingekuwa CDM wamepiga risasi kama walivyofanya ccm sijui wangekuwa wapi wote lupango na case kibao lakini mwajiri wake ndio kafanya hasemi, kwa ujumla hana jipya wala mvuto.

    ReplyDelete
  10. Tendwa huna lolote...ni wale wale tu tunawajua wote....Tanzania hakuna mgawanyiko wa madaraka (separation of powers) kati ya Serikali, Bunge na Mahakama. Vyote vimeshaingiliwa na siasa za serikali tawala. Tumeona na bado tunaendelea kuona Mahakama ikifanya maamuzi ya kisiasa badala ya kisheria na huko Dodoma kwa sasa BUNGE LA CCM linaendelea na mjadala wa sheria ya kuanzisha KATIBA YA CCM na sio KATIBA YA NCHI. Kwa sasa Tendwa, naomba na uwaambie wenzako, Watanzania wanaelewa kila kitu na wamechoka kudanganywa.....hakuna Mtanzania mjinga tena kila mtu anajua kusoma, kuandika na kuchambua issues enzi za kudanganya na maneno hewa imepita....Hivi hili bado hamjaligundua tu? Kama sio CHADEMA maovu ya CCM yangekuwa yanaendelea hadi sasa huoni wameanza hata kujivua magamba?

    ReplyDelete
  11. Nilitegemea msajili aeleze kama mahakama zinatumiwa/kuelekezwa kutotenda haki, vyama vifanye nini? bila kuwa na jibu la swali hilo vurugu haziwezi kuepukwa. Kila mwenye uwezo wa kufikiri na kuona yanayoendelea anajua kwamba mahakama zetu sio huru.

    ReplyDelete
  12. Naomba nimweleze Tendwa na wenzake anaowatetea kuwa " Bila haki hakuna sheria yoyote iliyo halali na wananchi hawana sababu ya kuzifuata{If there is no justice, the validity of the laws varnish!")
    Kwa hiyo kabla hajazungumzai mihimili, azungumzie kwanza haki katika sheria anazozisema ndipo awe na uhalali wa kuzungumza.

    ReplyDelete
  13. varnish!!!!!!!!!!! tehtehtehtehteh wajuaji mnaboa Kapate elimu ya watu wazima kwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...