Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Getrude Mpaka (kulia) akikabidhi zawadi za Idd El Hajj zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa kituo cha watoto yatima cha Tosamaganga Iringa leo.
Na Francis Godwin,Iringa
RAIS Jakaya Kikwete ametuma salama za Idd El –Hajj kwa watoto yatima mkoani Iringa ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi mbali mbali zenye dhamani ya shilingi 555,000 kwa kituo cha watoto yatima cha Tosamaganga wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa huku akitaka jamii kuendelea kuwasaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu .
Akikabidhi msaada huo leo kwa niaba ya Rais Kikwete katibu tawala wa mkoa wa Iringa Bi.Mpaka alisema kuwa zawadi hizo ni ishara ya upendo wa mheshimiwa Rais kwa watoto yatima na watanzania kwa ujumla bila kuwabagua kwa matatizo yao.
Hata hivyo alitaka jamii kuendelea na mshikamano wao kwa watoto yatima hao na kuepuka kuendelea kuwabagua watoto hao kutokana na matatizo yao na kuwa serikali itaendelea kuwasaidia watoto hao yatima kupitia vituo hivyo huku akiwataka wananchi kuendelea kushiriki kuwasaidia watoto hao.
Mpaka alizitaja zawadi zilizotolewa na Rais Kikwete kuwa ni pamoja na Chakula kwa maana ya mchele ,kilo 150 ,mbuzi watatu, mafuta ya kula lita 40 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 500,000.
“Nimekuja hapa kufanya mambo makubwa mawili jambo la kwanza kutoa zawadi na pili kuwafikishia salamu za Idd Al Hajj kutoka kwa mheshimkiwa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mheshimiwa Rais anawatakia heri na Fanaka kwa Idd El Haj,yeye amefarijika sana kushiriki nanyi kusherekea sikukuu hii ya Idd El Haj na alipenda kuwa nanyi hapa lakini kutokana na majukumu kuwa mengi ametuma salamu za kuwatakia heri na fanaka kwa Idd El Hajj na kuwataka watoto wote kusherekea sikukuu kwa furaha ,amani na kwa kudumisha upendo”
Akishukuru kwa zawadi hizo kutoka kwa Rais mkuu wa kituo hicho cha Tosamaganga Helena Kiwele alisema kuwa wamepokea msaada huo kwa furaha kubwa huku akidai kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 1969.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...