Asalaam alaykhum wajina,

Toka jana hakuna mafuta aina ya petroli huku mjini kwetu mtwara nzima tumehangaika mpaka leo alfajiri lori la gapco liliposhusha mzigo na watu kuanza kugombani ilikua ni patashika na foleni kubwa ya bajaji, pikipiki
magani na jamaa wenye vidumu. Huduma zilisimama kabisa kwa tax, piki piki na bajaji leo ilikua ni mwendo wa kupiga mguu tuu. Watu wapo katika foleni kuanzia saa 12 asubuhi mpaka sasa hajapata hayo mafuta
foleni ilivyondefu.

Chakufurahisha zaidi alitokea dereva mmoja wa piki piki na ngona na kuanza kutandika ngoma za kimakonde na waliokua katika foleni kuanza kuyarudi mangoma ya kimakonde.

Mdau Mtwara
Watu wenye Vidumu wakiwa kwenye foleni ya kupata kiwese.
Bajaj zimeaumua kutulia tu humu,maana haziwezi kwenda kokote kutokana na hali ya upatikanaji wese mkoani mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...