Mchezaji wa Timu ya Pool ya Taifa,Charles Venance akijiandaa kupiga moja
ya mipira ya pool katika mchezo wa kujipima nguvu na Timu ya Pool ya
Mkoa wa Iringa wakati Timu ya Taifa iliposimama mkoani hapo wakati
ilipokuwa safarini kuelekea nchini Malawi kulikokuwa kufanyike Mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011 ambayo kwa sasa yameahirishwa kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo hivi sasa.Timu hiyo kwa sasa ipo Mkoani Dodoma,ambapo leo itacheza mchezo mwingine wa kirafiki na timu ya mkoani hapo na baadae kuelekea Manyara,Arusha,Kirimanjaro na Tanga wakati ikisubiria taarifa rasmi ya nchi gani Mashindano hayo yatakapofanyika.
Mchezaji wa Timu ya Pool ya Taifa,Mohamed Iddi akijiandaa kupiga moja ya mipira ya pool katika mchezo wa kujipima nguvu na Timu ya Pool ya Mkoa wa Iringa wakati Timu ya Taifa iliposimama mkoani hapo wakati ilipokuwa safarini kuelekea nchini Malawi kulikokuwa kufanyike Mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011 ambayo kwa sasa yameahirishwa kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo hivi sasa.
Mchezaji wa Timu ya Pool ya Taifa,Abdallah Hussein akipiga moja ya mipira ya pool katika mchezo wa kujipima nguvu na Timu ya Pool ya Mkoa wa Iringa wakati Timu ya Taifa iliposimama mkoani hapo wakati ilipokuwa safarini kuelekea nchini Malawi kulikokuwa kufanyike Mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011 ambayo kwa sasa yameahirishwa kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo hivi sasa.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Pool ya Taifa wakifuatilia moja ya michezo yao kwa makini pamoja na Kocha wa Timu hiyo,Dennis Lungu (kulia).
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kufutwa kwa mashindano ya 'ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI' yaliyotarajiwa kuanza Novemba 22, hadi 26, 2011.
Akitangaza mabadiliko ya safari hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa Pamoja na mashindano hayo kufutwa Bia ya Safari, imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ifuatayo ya Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga baada ya kushauriana na chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Malawi.
Aidha imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa mashindano hayo kufanyika Malawi kumefuatia kutokea kwa machafuko ya Kisiasa na hii itatoa nafasi kwa mikoa iliyotajwa kuiona timu yao ya Taifa na baadhi ya wachezaji wakali wa mikoa hiyo kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wa timu yhiyo ya Taifa.
Akizungumzia na mtandao huu kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya 'ALL AFRICA CUP –MALAWI' yamefutwa kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wa chama cha pool Africa lakini tumefarijika sana kuona kwamba Bia ya Safari Lager bado iko na sisi bega kwa bega na kuipa nafasi timu yetu kufanya ziara ya michezo ya kirafiki na timu za mikoa’’ alisema katibu.
Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema “ Tulipokea taarifa za kufutwa mashindano kwa masigitiko makubwa sana kwani tulikuwa tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo, lakini nilifarijika sana kusikia kuwa wadhamini wetu SAFARI LAGER wametupa nafasi ya kujiandaa zaidi kwa kutupa michezo ya kirafiki katika mikoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...