Picha ya Marehemu Mary Ndehani Lista.
Wanafunzi wakiTanzania waishio na kusoma Bangalore wakiimba nyimbo za msiba wakati wa misa.
Wadada wakisikiliza neno la siku hiyo lililosomwa na kuhubiriwa na Makamu mwenyekiti wa jumuiya Bw. Anase Stephen na historia fupi ya Marehemu iliyosomwa na Msemaji mkuu wa jumuiya Bwana Aldo Kamugisha (hawapo pichani)
Shangazi wa Marehemu mama Esnath Mwakisale, alikuwepo kujumuika kwenye misa hiyo pamoja na wanafunzi wenzake Marehemu.
Viongozi wa TASABA (kutoka kushoto) Katibu Bi. Edna Stephen, Msemaji Bw. Aldo Kamugisha na Makamu wa Rais Bw Anase Stephen wakijadiliana na kuratibu shughuli nzima ya msiba wa mwanajumuiya mwenzao.
Rais wa wanafunzi waTanzania wasomao na kuishi mji wa Acharya India, Bi. Sira Mhogele akiongoza misa kwa nyimbo na mapambio.
Captain wa timu yetu ya mpira wa mguu na kiongozi wa jumuiya kwa jimbo la Gubi, Bw. Freddy Matthias ( mwenye rozari) akiongoza waTanzania kuimba nyimbo za msiba.
Uongozi wa TASABA (Tanzania Students Association - Bangalore ) na familia ya Marehemu, unatoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki pamoja nasi katika kipindi kigumu tulichopitia cha kuondokewa na mwanafunzi mwenzetu Bi. Mary Ndehani Lista ( 25 ) aliyetwaliwa na Mungu tarehe 07-11-2011 ( baada ya kuugua Ovarian na Colon Cancer kwa miezi mitano ), kusafirishwa na kuzikwa nyumbani kwao Dodoma.
Tunazidi wapa pole ndugu wote wa karibu walioguswa na msiba huu, marafiki na jamaa wote, hakika Pengo la dada yetu sio rahisi kuzibika, lakini twaamini ya kuwa ameenda pumzika na iko siku tutajumuika naye pamoja Mbinguni, twamwomba Mungu awafarijini nyote.
Tunawashukuru wanafunzi waTanzania wote wasomao na kuishi Bangalore kwa moyo wa upendo, umoja na kushirikiana vyema kuanzia kipindi dada yetu Mary alipoanza kuugua mpaka Mungu alipomtwaa hadi kwenye misa ya kumkumbuka na kumwombea, Kipekee tunawashukuru dada Suzan O. Kavishe na bi Esther Bugoya kwa kujitolea nyumba zao kwa ajili ya kufanyia ibada ya kumkumbuka mwenzetu. Pamoja na viongozi wa jumuiya yetu waliojitolea kwa hali na mali kufanikisha shughuli zote katika kipindi hichi kigumu.
Aidha tunapenda kuwashukuru ndugu zetu wote wenye blogs mbalimbali kwa kutusaidia kufikisha ujumbe kwa waTanzania wenzetu wote popote pale walipo ulimwenguni.
Mwisho kabsa tungependa waomba wa Tanzania tuzidi kuombeana sisi kwa sisi, na kuishi vyema kwani hakuna ajuaye kesho ina nini, leo hii ni yetu bali kesho sio yetu ni ya Mungu.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Makamu wa Rais - TASABA
Mr. Anase Stephen
Masters of Commerce - Accounts & Finance
Jain University, Jayanagar - Bangalore.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI NA AWABARIKI NYOTE ..AMEN
ReplyDeleteMwanafunzi mwenzenu -UK
POLENI SANA DADA NA KAKA ZETU MLIOFIKWA NA MSIBA, NA PIA WANA FAMILIA WOTE. DADA YETU AMETANGULIA KWA MUUMBA WETU, NASI TUTAFUATA. TUPOPAMOJA NAYI KUMUOMBEA ILI MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI.
ReplyDeletePOLENI SANA NDUGU ZETU.
Wanafunzi wenzenu - RUSSIA
inatia uchungu sana kuona binti mdogo kama huyu amechukuliwa kwa gonjwa kubwa kama hili, ama kweli kama alivyoandika huyo kaka, Hakuna ajuaye kesho ina nini, leo ni siku yetu, kesho siku ya Mungu.
ReplyDeleteMungu ailaze pahala pema peponi roho ya marehemu.
Pia nawapongeza wanafunzi huko Bangalore kwa kuweza kushirikiana vyema, ama kweli ni jambo la busara mno.
mbeba boksi.
Poleni sana! Bwana alitoa, na bwana ametwaa! Jina lake lihimidiwe. R.I.P Mary. You have gone to the place where everyone has to go.
ReplyDeleteMwanafunzi mwenzenu-KTH (Sweden)