Na Anna Nkinda – Maelezo

Shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-NAKAYAMA iliyopo Rufiji mkoani Pwani imepokea msaada wa vitabu 1000 kutoka kwa Taasisi ya British Charity READ International ambayo inafanya kazi ya kukusanya vitabu nchini Uingereza na kuvigawa katika nchi za Afrika.

Vitabu hivyo vimekabidiwa leo kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Mendeleo (WAMA) inayomiliki shule hiyo na Hana Mitchell Mtendaji mkuu wa shirika hilo mbele ya Duchess of Cornwall Camila Parker Bowles katika viwanja vya WAMA jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi vitabu hivyo Mitchell alisema kuwa Read International na vijana wake 1000 wamekuwa wakitoa material ya elimu kwa zaidi ya vijana nusu milioni ndani ya shule 1000 katika mikoa 14 hapa nchini kwani kupatikana kwa elimu kunamsaidia mtu kupiga mbele hatua moja na hivyo na kujikwamua na umaskini.

“Kuwepo kwenu hapa kunaonyesha kazi kubwa ya watu wanaojitolea katika Nchi za Tanzania na Uingereza kwani nchini Tanzania wanafunzi wanachangia kusoma kitabu kimoja lakini Taasisi yetu inafanya kazi ya kuhakikisha kuwa inatoa vitabu viwili kwa kila mtoto aliyeko shuleni ambaye atavisoma na kuvifurahia”, alisema Mtendaji Mkuu wa Read International.

Aliendelea kusema kuwa vijana kutoka Tanzania na Uingereza wanafanya kazi kwa pamoja ya kubadilisha maisha yao kwa kitabu kimoja kuweza kuondoa ujinga kwa vijana zaidi ya 1000 kwani wanaondoa tofauti kwa vijana hao kwa kuwapa nafasi mbalimbali.

Kwa upande wake mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuwa washirika wakubwa wa kuboresha elimu kwa miaka mingi na kuhakikisha kuwa vitabu vinapatikana kwa watoto wa Tanzania.

Mama Kikwete alisema, “Vitabu tulivyovipata leo vitawaongezea ujuzi wanafunzi wetu wa WAMA-NAKAYAMA kwani ninauhakika kuwa vitawasaidia kufahamu mambo mbalimbali katika masomo yao na tutavitumia kwa manufaa ya shule yetu”.

Mama Kikwete alikabidhiwa kitabu kimoja na Princess Camila kitabu ambacho kilikamilisha jumla ya vitabu milioni moja vilivyotolewa na Read International ambayo ni taasisi ndogo ya kujitolea ya Waingereza inayofanya kazi ya kukusanya vitabu kupitia maelfu ya vijana wanaojitolea na kuvisambaza katika shule mbalimbali hapa nchini.

Duchess of Cornwall Camilla alikutana na wanafunzi walionufaika na mradi huo kutoka shule ya Sekondari ya Kilakala pamoja na wanafunzi watakaonufaika na mradi huo kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA – NAKAYA.

Camila ameambatana na mme wake Prince Charles katika ziara yao ya siku nne ya kutembelea Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa wao, wakipewa misaada waitoe kwa shule zisizojiweza.

    ReplyDelete
  2. Asante sana Anna Nkinda kwa habari, Mama JK,wewe kweli wewe ni mwalimu..haya ndiyo mambo tunayotaka kuyasikia na kuyaona First Lady akiyafanya.hakuna urithi mzuri kama Elimu.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...