Sabal Kheir ustaadh Michuzi

Mimi nilikuwa nauliza

kwa nini ukifanya U-turn kwenye traffic lights au sehem ambako una uwezo wa kufanya U turn polisi wanakukamata?

Nijuavyo mimi matumizi ya barabara yanaendana na sheria na alama za barabarani. Sasa kama hakuna sehem iliyoonyesha tusifanye U-turn halafu mtu ukafanya U turn je kosa ni la dereva au la jamaa wa usalama wa barabarani kutoweka signs?

Nazungumza kama Mtanzania aliye nje ya nchi na huku niliko (ulaya) kama hakuna bango au alama inayokataza jambo bas mtu unaruhusiwa tuu kufanya hicho kitu

naomba akipatikana mtu toka usalama wa barabarani atuhabarishe tafadhali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sifahamu ni nchi gani ya ulaya ulipo ila sign za barabara sio tu vibao vya kuweka pembezoni mwa barabara angalia chini ya barabara (lami) pia kuna signs. Ukifika kwenye mataa kuna alama chini zinakuambia nini cha kufanya kwenye lane husika uliyopo.

    Ila naweza kukuhakikishia hakuna barabara yoyote unayoruhusu kufanya u-turn sehemu yeyote kama hiyo barabara inafuata standards. Na hili ni kwa dunia nzima. kama utakuwa unafanya hivyo sehemu yoyote au nchi yoyote utakuwa unafanya makosa na hiyo nchi haipo makini.

    ReplyDelete
  2. CCM ISIWE KIGEU GEU

    ReplyDelete
  3. Tanzania hatuna U-Turn ndio maana unakamatwa. read your road signs!

    ReplyDelete
  4. Wewe anonym wa kwanza napenda kuhakikishia umma kwamba hujatoka nje ya Tanzania. Alichekisema jamaa aliyeuliza swali ni ukweli mtupu na wenzetu wanapiga U-turn hata katika traffic light endapo alama hiyo haipo. Una maana kwamba Tanzania wanajua sheria kuliko Ulaya? Usibishe kitu ambacho hujui. Mimi naomba mwana usalama ajibu kwa nini Tanzania unakamatwa hata kama hamna alama ya U-turn/

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa kwanza kabisa umejitahidi sana kutetea nchi yetu. Hongera sana. Lakini aliyetoa malalamiko bado yupo sahihi. Kuna sehemu hakuna kabisa alama yeyote iwe kibao au yakuchowa barabarani inayozuia kipiga U-Turn. Na ukipiga U-Turn bado unakamatwa. Ukiuliza mbona hakuna alama yeyote inayozui kupiga U-Turn, polisi naye anakuuliza kwani kuna alama yeyote inakuruhusu kupiga U-Turn? Halafu ukiwaonyesha international drivers license na pasport ya Marekani wanafoka kwa sauti "POTEA!". Mbona polisi wa Ulaya na Marekani ukiwaonyesha international drivers license na pasport ya Tanzania hawakuambii upotee?

    ReplyDelete
  6. Sikubaliani na Mdau aliyeandika "naweza kukuhakikishia hakuna barabara yoyote unayoruhusu kufanya u-turn sehemu yeyote kama hiyo barabara inafuata standards. Na hili ni kwa dunia nzima. kama utakuwa unafanya hivyo sehemu yoyote au nchi yoyote utakuwa unafanya makosa na hiyo nchi haipo makini"!!

    Ningekubaliana na wewe kama ungesema kuwa "it's rare kuona kibao cha U-turn kwenye junction au traffic signal" Nasema hivyo kwa sababu nimeshaona kibao cha U-turn kwenye traffic signal, na kulikuwa na sababu maalumu ya kukiweka pale. it would be a long story kuelezea ni kwa nini kiliwekwa. Lakini as long hakuna kibao kilichoonyesha no U turn na barabara imegawanywa (center median), then unaruhusiwa ku-U-turn kisheria.

    ReplyDelete
  7. Kimsingi. Dunia nzima inaruhusu U-turn penye junction unless kuna sign inayokataza hivyo. Polisi njaa tu ndio maana wanasumbua sumbua.
    Hapa Bongo kuna vitu vya kiajabu ajabu vinatokea bila sensible explanation....eti hapa ni BONGO, itumie uwezavyo!

    ReplyDelete
  8. kwa nini wana usalama wa barabarani hawaji kutujuza sisi wananchi?

    wanaogopa nini?

    michuzi naomba uiweke juu hii mpaka kupatate suluhu ya hili jambo

    ReplyDelete
  9. Wewe unaesema hakuna alama yoyote duniani inayoruhusu u-t!!! unacheza hebu badili katiba yako haraka ili uone nchi ngapi zinaruhusu. usibweteke!!!

    ReplyDelete
  10. Naomba thread iwe top ili wana usalama barabarani waje kutuweka sawa juu ya hili


    tafadhali sana bwana michuzi

    ReplyDelete
  11. Huyu anayesema hamna nchi yoyote duniani inaruhusu U-Turn hajawahi toka nje ya Tanzania, ni vema mtu u-comment out of experience, hapa marekani kama hamna kibao kinakataza unapiga U-turn popote pale, na hata UK nimeona hivyohivyo, hiyo ni part ya exposure kwa watu tuliosafiri, mwana usalama aliyeishi nje anaweza jibu hili vizuri otherwise tunatwanga maji kwenye kinu tu.

    ReplyDelete
  12. This link might help some of us. http://en.wikipedia.org/wiki/U-turn

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...