Timu ya Taifa (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Novemba 3) kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 jijini N'Djamena. Wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini kesho, isipokuwa wale wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi ambao wataanza kuingia nchini Novemba 4 mwaka huu.
Kambi ya Taifa Stars itakuwa hoteli ya New Africa na mazoezi yatafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kulingana na programu za Kocha Mkuu wa timu hiyo Jan Poulsen. Timu inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 8 usiku kwenda N'Djamena.
Waamuzi wa mechi ambao wote wanatoka Nigeria ni Bunmi Ogunkolade, Tunde Abidoye, Baba Abel na Abubakar Ago. Mtathimini wa waamuzi atakuwa Idrissa Sarr kutoka Mauritania wakati Kamishna wa mchezo huo ni Hamid Haddadj (Algeria).
TFF,Wachezaji,walimu kuweni na Malengo mapema kama wenzetu wanavyofanya..siyo mnaenda jijini N'ndjamena bila mpangilio Hii mechi ni ya mtoano..'Vision' iwe kuiondoa Tchad-iwe kwa penati au nini.Tusikubali kupoteza huo mchezo wa nje.Tchadi wako chini kwa viwango vya FIFA lakini hakuna dharau hapa.Kuingia kwenye hilo kundi la kombe la Dunia ni kazi kubwa sana.Tukiwatoa Tchad kuna kupambana na Mshindi kati ya Burundi na Lesotho ndiyo twende kwenye makundi..Siyo kazi rahisi..
ReplyDeleteDavid V
Inaonekana njia ya Simba sasa ndo imefunguliwa rasmi na Yanga, wengine wanapita tu !
ReplyDeleteWendawazimu ni hali ya kurudiarudia kitendo na kutegemea matokeo tofauti. Babu hatufikishi popote huyo, bora Maximo maradufu.
ReplyDeleteLakini mbona sioni na wala sijasikia timu ya Taifa kujipima nguvu na nchi nyingine kabla ya mechi. Hawa wachezaji wanatoka timu tofautitofatuti hivyo wanahitaji mechi za majaribio ili kocha ajue namna ya kuwatumia wachezaji wake pia hata wao wazoeane kiuchezaji>
ReplyDelete